·
Ni katika kwa watoto na vijana hapa nchini
·
Ni wakati wa mapambano ya
Haleluya na Yanga
·
Askofu Dk. Mtokambali
azitabiria makuu timu za Tanzania
Mkakati wa uinjilisti ulioasisiwa
na kanisa la Tanzania Assemblies of God kupitia Idara zake za Christian
Ambassadors Student Fellowship
Tanzania(CASFETA) , Idara ya watoto na Vijana, umemgusa Waziri wa Serikali ya
Magufuli na kuipongeza.
Akiongea wakati wa Mchezo
uliohusisha Timu za mpira wa miguu Haleluya kuotoa Korea na Yanga Junior, ya hapa nchini, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk. Harson Mwakyembe alisema kanisa
limefanya jambo linaloipa sifa nchi hii kwa mataifa mengine.
Dk. Mwakyembe akihutubia wakati wa
mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa mpira wa mguu wa Uhuru jijini Dar es
Salaam, alisema serikali inaishukuru kanisa la TAG kwa juhudi zake
Aidha alisema kuwa ujio wa timu
hiyo ya Haleluya iliyokuja hapa nchini chini ya Mwamvuli wa kanisa la TAG ni
umetangaza baraka kwa taifa la Tanzania.
Aidha Waziri huyo alisema kufika
kwa timu hiyo nchini, haikuwa tu kuitangaza soka la Tanzania kimataifa, bali pia
ni kuimarisha urafiki kati ya Tanzania na Korea uliodumu kwa zaidi ya miaka 25.
Tuanatoa shukurani kwa Kanisa la
TAG chini ya Askofu Dk. Barnabas Mtokambali, kwa kuwezesha timu
hiyo ya korea kuja hapa nchini na kufanikiwa kucheza na Yanga Junior,” alisema
Dk. Mwakyembe na kuongeza:
“Tunaimani kuwa kupitia mchezo huu
umoja na mshikamano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea utaendelea kudumu na
kuwa na tija kwa mataifa mawili.”
Hata hivyo waziri huyo alitoa wito
kwa Watanzania wengine kuiga mfano wa kanisa la TAG katika kuzingatia mambo ya
msingi yanayotangaza taifa kwa mataifa mengine duniani.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa
Kanisa la TAG, Dk. Baranabas Mtokambali aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa mechi
hiyo alisema mkakati wa mchezo huo ni kuileta Tanzania kwenye Kombe la dunia.
Dk. Mtokambali alisema, kanisa la
TAG limeamua kuunga mkakati huo kwa vitendo zaidi kwa kuileta timu ya Haleluya
ya korea kucheza na timu ya Yanga ya Tanzania.
Aida Kiongozi huyo wa kiroho
alisema kuwa, pamoja na mchezo huo lakini pia kanisa linatumia furasa hiyo
kufanya uinjilisti ili kuwaleta watu kwa Yesu.
Tutacheza mchezo lakini pia
tutahubiri na injili, hii siyo burudani, au mazoezi ya kujenga mwili kiafya, au
kujenga ushirikiano tu, ni njia mojawapo ya kuinjilisha,” alisema Dk.
Mtokambali.
Dk. Mtokambali alitumia fursa hiyo
kuitabiria mambo makubwa timu za hapa nchini akisema kuwa kwa michezo hiyo
itaanza harakati zake za kuifikia kombe la dunia.
Sanjari na mchezo huo wa kirafiki
ambao timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, lakini pia uongozi wa kanisa
la TAG na ushirika wa Korea ulikabidhi jezi pamoja na mipira ya miguu kwa
Waziri huyo kwa ajili ya timu hiyo.
Kanisa lilitumia furasa hiyo
kuhubiri mara baada ya mchezo huo kumalizika na kuafanikiwa kuongoza sala ya
toba kwa watoto na watu waliohudhuria kutazama mpirab huo.
Aliyehubiri injili ya dakika 15
mara baada ya mechi kumalizika alikuwa na Mkurugenzi mkuu wa Watoto wa kanisa
la TAG, Mchungaji Godwin Mjaki.
Mchungaji Mjaki alisema kuwa Mungu
ameandaa mpango mzuri kwa ajili ya watoto na kwamba anawahitaji waishi maisha
ya kumtegemea yeye.
Mchezo huo wa mpira kati ya Yanga
na Haleluya sport club ya Korea, iliandaliwa na kanisa la TAG mahususi kwa
ajili ya kupenyeza injili na karama kwa watoto.
Mechi hiyo ilihudhuriwa na watoto
zaidi ya 13,000 kutoka katika makanisa
ya TAG jijini Dar es Salaam, huku wengine ni ni kutoka shule mbalimbali za
msingi hapa jijini.
Mchezo huo pia ulihudhuriwa na baadhi ya maaskofu wa kanisa la TAG, na
makanisa mengine Wachungaji na wakurugenzi wa Idara wakiongozwa na Mkurugenzi
wa CASFETA Mchungaji Huruma Nkone ambaye ndiye alikuwa mratibu mkuu.
0 comments:
Post a Comment