·
Yadaiwa kuandaliwa na kundi la watu wenye nia
mbaya na Ukiristo
RASIMU tata ya katiba inayodaiwa kuandaliwa na
kikundi fulani cha imani dini ya kiislamu ikishirikiana na dhehebu moja imeibua
mtafaruku mkubwa huko Geita kwa baadhi ya Wachungaji na kugoma kuisaini.
Wachungaji waliogoma
kuisaini ambao walifamikiwa kuongea na gazeti hili wameelezwa kuwan ni wa
Katoro na Busesele Wilaya ya Geita mkoani humo.
Watumishi hao wa Mungu
wamedai wamegoma kuisaini na kuipitisha kwa vile wamebaini ndani yake kuna
vipengele vinavyoashiria ubaguzi wa kidini katika baadhi ya maamuzi.
Utata unaoonekana katika
rasimu hiyo ya katiba ni pamoja na kuwapa waumini wa dini ya kiislamu rhusa ya pekee kwamba ndiyo wenye mamlaka ya
kuchinja jambo ambalo wachungaji hao
wamelikataa kutokana kwamba suala hilo ni la kiimani zaidi.
Jambo jingine ambalo
walilielezea kuwatia shakani ni
kutoruhusiwa kufuga nguruwe katika maeneo hayo jambo ambalo wanaamini kama
likipitishwa linaweza kuleta mgogoro mkubwa hapo baadaye.
Katoro ni sehemu ambayo
kuliwahi kutokea mgogoro wa nani wenye mamlaka ya kuchinja
kati ya wakristo na waislamu na kusababisha kifo cha Mchungaji…….
Akizungumzia tukio hilo
mmoja wa wachungaji waliodai kugoma kusaini rasimu hiyo Michael Boaz alisema sababu
ya kugoma ni kutokana na utata uliomo ndani ya rasimu hiyo ambayo wameshindwa
kuyaelewa.
Mchungaji Boazi alisema
kitu kingine kilichomfanya asisaini ni kwamba walikuwa wachache kwenye kikao
kitu ambacho aliogopa kutoa maamuzi ya wengi kwa watu wachache.
Lakini pia jambo jingine
ni kwamba hakujua rasimu hiyo ya katiba imeandikwa na nani na imetoka wapi.
“Mimi sijui nani
aliyeandika rasimu hiyo ya katiba hii hivyo nimeshindwa kuamua nisije
nikaamulia matatizo watu ninaowaongoza” alisema mchungaji huyo na kuongeza:
“Halafu tulikuwa wachache
hata hivyo niliwaacha waendelee na kikao chao mimi nikaondoka.”
Mwenyekiti wa Makanisa ya
umoja wa kipentekoste mkoa wa Geita Emanuel Peter wa kanisa la FPCT alisema
kuwa taarifa hizo amezisikia na yeye kwa upande wake hakubaliani nazo.
Alisema alisika juu juu
taarifa hizo lakini kwa sasa yuko safarini akirudi atafatilia kwa undani zaidi.
Kiongozi huyo wa kiroho
alisema, kitu anachofahamu kuwa kuna mradi wa uchimbaji wa visima ulioibua sintofahamu katika maeneo hayo.
Mradi huo unaitwa Mradi wa
Amani ambao umepitia katika kanisa la KKKT.
Mwenyekiti huyo
alibainisha kuwa, Wachungaji wameshindwa kuelewa mradi una nia gani na ndiyo
maana wameshindwa kusaini rasimu ya katiba ya mradi huo.
Kiongozi huyo alisema, katika maeneo ya
Buselesele na Katoro kuna migongano mbalimbali ya kiimani lakini wanamwamini
Mungu atawatetea.
Alibainisha kuwa migongano
hiyo ni kati ya Imani ya kikristo na kiislamu.
Aidha alisema kuna mbinu
mbalimbali zinatumika ili kuhalalisha kuwepo kwa kukandamizwa kwa Imani moja.
“Kumekuwa na lugha raini
na za uongo ambazo zimekuwa zikizungumzwa ili kukandamiza Imani moja lakini
tunamshukuru Mungu huwa anatusimamia” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa;
“Mimi nashangaa malumbano na migongano inatoka wapi
kwani tuna haki mbele za Mungu na taifa kufanya mambo yetu kwa Imani ya dini
yetu”
Hata hivyo Mwenyekiti huyo aliwataka wachungaji na
wakristo kwa ujumla kutafuta maarifa ya kusoma neno la Mungu na katiba na mambo
mbalimbali yanayoendelea duniani ili wajue mambo mengi yatakayowasaidia kuvuka
katika vikwazo dhidi yao.
Jibu la Maisha lilimtafuta Mkurugenzi wa mradi huo
David Mbwambo alisema kuwa, mradi huo uko kupitia kanisa la KKKT Dayosisi ya
Kanda ya Ziwa Victoria.
Alisema, lengo kubwa la mradi huo ni kuisaidia jamii
na kuwaleta wananchi kuishi kwa umoja, upendo na mshikamano wa sehemu hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, wanafanya hivyo
kwasababu katika maeneo hayo kumekuwa nakutoelewana baina ya Imani mbalimbali
hasa mbili Kiristo na Kiislamu.
Alibainisha kuwa, tofauti zao zinfanya watu hao
wasiishi kwa Amani wala ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kijamii.
“Sisi wote ni wamoja sasa siyo vizuri kuona watu ni
majirani halafu hawashirikiani vizuri” alisema mkurugenzi na kuongeza;
“Unajua ujirani mwema ni kitu kizuri kwasababu mtu
anaweza kutafuta rafiki lakini siyo jirani sasa unaona umuhimu wa jambo hilo.”
Kuhusu rasimu ya katiba ya mradi huo alisema kuwa,
anawaachia watu wanaoishi maeneo hayo kutunga na kubainisha mambo ambayo
watakubaliana nayo na kuishi kwa amani kama watu wa mahali pamoja.
Alisema hata hivyo anafatilia kila hatua na
anafahamu nini kimeandikwa katika rasimu hiyo ya katiba na kwamba iko sawa.
Lakini alipotakiwa kutoa au kuonyesha mambo
yaliyokuwepo kwenye rasimu hiyo Mkurugenzi huyo alisema kuwa, hawezi kutoa
kwasababu bado hayajawekwa sawa.
Alipoulizwa hiyo waliyopewa wachungaji na mwenyekiti
wake wasaini alisema hafahamu wao hawajatoa bali wapo katika harakati za mwisho
kuitoa.
KUMRADHI
Tunaomba kuweka sawa
wasomaji wa gazeti hili ambao kwa namna moja ama nyingine walipata usumbufu
kutokana na kichwa cha habari cha gazeti la wiki iliyopita kilichosomeka: SERIKALI YAHALALISHA NDOA YA JINSIA MOJA.
Ieleweke kwamba, habari hiyo
haikuhusiana kabisa na serikali ya Tanzania. Kwa wale waliosoma habari hiyo
ndani walielewa ukweli huo. Usahihi ni kwamba, habari hiyo ilihusu serikali ya
SWEDEN na siyo ya Tanzania. Msimamo wa
gazeti hili ni kwamba haliungi mkono wala kushabikia vitendo viovu kama NDOA ya
jinsia moja vinavyotokea kwa mataifa ya Ulaya. Bado tunaisihi serikali yetu
kupinga vitendo hivyo visiingie hapa nchini.
Kongamano la Mashariki Kusini laacha historia
Na Denis Massawe
KONGAMANO la Jimbo la Mashariki
Kusini limeacha historia isiyofutika baada ya kuainisha maendeleo makubwa
waliyoyapata kwa muda mfupi tangu Jimbo hilo kuazishwa.
Akizungumza katika Kongamano hilo
lililofanyika katika kanisa la Mbagala Kizuiyani, Katibu Mkuu wa kanisa la
Tanzania Assemblies of God, Mchungaji Ron Swai, ambaye alimuwakilisha Askofu
Mkuu wa kanisa hilo, alikubali kasi kubwa ya jimbo hilo.
Katibu huyo alibainisha kuwa,
maendeleo ambayo Jimbo hilo limeyapata ni yakustaajabisha kwani ni makubwa
ukilinganisha na umri wa Jimbo hilo tangu lilipozaliwa.
Licha ya Katibu huyo kuonesha
kustaajabishwa na maendeleo hayo ya muda mfupi katika Jimbo hilo, vilevile aliwapa
mbinu ya kuweza kuufikia Mpango Mkakati wa Kanisa hilo unaobebwa na kauli mbiu
ya ‘Miaka Kumi ya Mavuno Tanzania Kwa Yesu.’
“Mimi nawapa utundu mwezenu kabla
sijatoa neno la Mungu kanisani kwangu lazima niwaambie kwanza washirika wangu
waulizane wenyewe kwa wenyewe je umemvunia nini Mungu wiki iliyopita? na Je,
umemtumia nani ujumbe kupitia simu yako aje kanisani?” Alisema Rev. Ron Swai.
Katibu huyo alibainisha mambo
kadhaa ambayo yalitoka katika meza ya Askofu Mkuu wa kanisa hilo, ambayo ni
kumtaka kila mchungaji kubainisha mali za kanisa na zake binafsi, kuandaa
taarifa, taarifa kuhusu mfuko wa hifadhi ya jamii pamoja na kuhimiza makanisa
kujenga shule za chekechea, msingi na sekondari.
“Tafadhali pelekeni pesa zenu makao
makuu bila kuchakachua kuanzia sadaka, fungu la kumi pamoja na michango ya
Idara.” Aliongeza Swai.
Nae Askofu wa Jimbo hilo, Rev. Victor
Tawete, alisema kuwa, Jimbo hilo mpaka kufikia Januari mwaka huu, lilikuwa na Sehemu(Section)
kamili nne.
Askofu Tawete alizitaja sehemu hizo kuwa ni; Temeke, Mbagala,Vikindu na Kibiti kwa upande
wa zinazoendelea alisema kuwa ni pamoja na Mkuranga, Rufiji na Mafia.
Tawete alisema kuwa wanamshukuru
Mungu sehemu za Mkuranga na Rufiji zimefanikiwa kuongeza makanisa na Wachungaji
na kwa sasa zimepandishwa kuwa Sehemu kamili.
“Jimbo letu limebakiwa na sehemu
moja inayoendelea ya Mafia yenye makanisa matano. Sehemu hizo zote zinaongozwa
na Waangalizi na kamati zao kwa mujibu wa katiba ya kanisa letu la Tanzania
Assemblies of God.” Alisema Tawete.
Askofu huyo alibainisha kuwa Jimbo
hilo lina Idara 10 zinazoongozwa na wakurugenzi na kamati zao. Idara hizo alizitaja
ni pamoja na Idara ya Wanawake Watumishi
wa Kristo (WWK), Wajumbe wa Kristo(CA’S),
Watoto, Uinjilisti, Umisheni, Maandiko na Uanafunzi, Elimu, Miradi, CASFETA na
CMF.
Jimbo la Mashariki Kusini
lilizinduliwa rasmi na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Rev.
Dr. Barnabas Mtokambali, Tarehe 27 mwezi wa 9 mwaka 2016.
Askofu Victor Tawete, aliwataja viongozi
wenzake katika jimbo hilo kuwa ni;
Makamu wake Rev.Samson Kametta na Katibu Rev.Weston Sambo.
Mpaka sasa Jimbo hilo limedhihirisha
kuwa ni imara baada ya kuanza kufanikisha malengo waliyokuwa wameyaweka.
Miongoni mwa malengo hayo ilikuwa
ni kuongeza makanisa ambapo walikabidhiwa Jimbo likiwa na makanisa 98 mpaka
sasa wameongeza 21 na kufanya wafikie 119.
Licha ya kuongeza makanisa lengo
jingine lilikuwa ni kuongeza idadi ya washirika ambapo kipindi wanapokea Jimbo
hilo lilikuwa na Washirika 9015 lakini mpaka sasa lina washirika 9761 ongezeko
likiwa ni washirika 746.
Kwa upande wa wachungaji walikuwa
104 lakini sasa wapo 120 ongezeko likiwa ni wachungaji 20 na upande wa
kusomesha watumishi Chuo cha kupanda makanisa mpaka sasa wanasomesha watumishi
35 huku chuo chao binafsi yaani cha Jimbo kikitarajiwa kuanza tarehe 15 mwezi
wa 7 mwaka huu.
Jimbo hilo limeshafanya shughuli mbalimbli
tangu kuanzishwa kwake miongoni mwake ni kufanya Ziara kwenye sehemu zote za
Jimbo zikiwemo za mafunzo ya taifa, baraza la watendaji, mafunzo ya uandishi wa
vitabu Dodoma, mafunzo ya uongozi(ILI) na semina elekezi za takwimu na mpango
mkakati.
Vikao vingine walivyoudhuria ni
kimoja cha tathimini cha baraza la waangalizi Jimbo pamoja na kusomesha
wanachuo wawili chuo cha Mtama.
0 comments:
Post a Comment