|
DONALD TRUMP |
|
Vladimir Putin |
Rais Mteule wa
Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na Raia wa Urusi Vladimir
Putin na pengine kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo. Trump
aliyasema hayo katika mahojiano yake na jarida la Wall Street yaliyochapishwa
hii leo ambapo alisema vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi vilivyowekwa na Rais
Barack Obama mwezi Desemba vitaendelea kuwepo angalau kwa kipindi fulani chini
ya utawala wake. Hata hivyo Trump alisema vikwazo hivyo vinaweza kuondolewa
iwapo Urusi itashirikiana na Marekani hususani katika kupambana na makundi ya
itikadi kali. Uhusiano kati ya Trump na Urusi umeibua mjadala nchini Marekani
mnamo wakati baraza la Seneti nchini humo likijiandaa kwa uchunguzi unaohusiana
na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa lengo la kumsaidia
Trump kushinda katika uchaguzi huo. Na kuhusiana na msimamo wa Marekani
kuhusiana na Taiwan Trump alisema majadiliano kuhusiana na suala hilo
yanaendelea.
0 comments:
Post a Comment