Maafisa wa Marekani wanaamini kwamba Korea kaskazini ilitekeleza jaribio jingine la mashine ya kurushia makombora yake.
Jaribio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Jumatano litakuwa jaribio la kwanza la mashine kama hiyo kutekelezwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Machi.
Habari hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi kati ya washington na Pyongyang kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea kaskazini.
Utawala wa Trump umefanya swala hilo kuwa swala kuu.
Licha ya shutuma za kimataifa ,Korea Kaskazini imeongeza majaribio yake ya makombora kwa lengo la kutengeza kombora linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Shirika la ujasusi la Marekani limeonya mwezi uliopita kwamba Korea Kaskazini linakaribia kufanikiwa katika mpango huo.
Maafisa wa Marekani waliokuwa wakizungumza na vitengo kadhaa vya habari walisema hatua hiyo ya hivi karibuni siku ya Alhamisi ni awamu ya kwanza ya kutengeza kombora la masafa marefu ambalo litaweza kufika Marekani.
Kutokana na kiwango cha siri cha vitendo vya majeshi yote ya Korea Kaskazini, ni vigumu kwa wataalam kuangazia hatua ilizipogwa na taifa hilo kutengeza kombora la masafa marefu.
Mashine hizo zinaweza kutumika katika kurusha satelaiti angani, lakini maafisa wa Marekani wana wasiwasi teknolojia hiyo inajaribiwa kutengeza kombora linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
0 comments:
Post a Comment