PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Jamii ya kabila la Wahdzabe wakiwa katika moja ya shughuli za utamaduni wao.


Mahmoud Ahmad Karatu

Hatimaye zoezi la kuwahesabu Wahadzabe waishio wilayani Karatu lafanikiwa kwa asilimia mia moja baada ya wanajamii kujitokeza kwa wingi  kuhesabiwa ambapo wameitaka serikali kutimiza ahadi zao wakati wa uhamisishaji ili kuona matokeo ya zoezi hilo.
Walionyesha furaha yao wakati wa kuhesabiwa baada ya kukabidhiwa nyama ya punda milia 15 kama ushawishi wa kujitokeza kuhesabiwa walisema kuwa wanaishukuru serikali yao hasa ya awamu hii kwa kuwakumbuka na kuona umuhimu wa wao kuhesabiwa.
Akiongea kwa niaba ya wenzake Martha Daniel alisema kuwa wao kama wao  ni jamii ambayo mara nyingi wamekuwa wakiishi porini na kutegemea matunda na wanyama wa porini ambapo kwa sasa wamevamiwa na makabila wengine na kuchunga mifugo yao na kukata miti katika makazi yao hali iliyosababisha maisha yao kuwa magumu zaidi.
Aliongeza kuwa kutokana na kuvamiwa na makabila hayo wamekuwa wakikosa chakula hali ambayo wamekuwa wakiishi mazingira ya shida sana hivyo wameiomba serikali kuwaamisha makabila mengine katika pori hilo wanaloishi au kuwatafutia eneo lingine watakalofanikiwa kupata matunda na wanyama pori ilivyokuwa mwanzo.
Hii ni moja ya Makazi (myumba) ya jamii ya kabila ya Wadatooga wanaoishi porini. Hawa nao ni Watanzania wanaoishi maisha bora kwa kila Mtanzania.(Picha na Joseph H. Ongong'a)



Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: