BREAKING NEWS
ASKARI wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linatuhumiwa kumpiga risasi muuza magezeti mkoani humo wakati wa kuwatawanya wafuaasi wa Chama Cha Maendeleo na Demokrasia Chadema.
Wanachama hao wa Chadema walikuwa wakiandamana kwenda uwanja wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na viongo wa kitaifa wa Chama hicho.
Taarifa zilizolifikia tovuti ya habari ya J$M;WAMOJA hivi punde zinadai kwamba muuza magezeti huyo hakuwa mwanachama wa Chadema wala hakuwa katika maandamano hayo.
Akizungumzia tukio hilo mmoja wa mashuhuda wa ghasia hizo alisema kwamba muuza magazeti huyo alikuwa kando kando ya barabra akiuza magazeti yake lakini gafla alipigwa risasi utosini na kutokea kwenye paji lake la uso na kufia hapo hapo.
Katika vurugu hizo Jeshi hilo la Polisi ililazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kurusha risasi ovyo kwa lengo la kuwatawanya wafuasi wa Chama hicho.
Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alisema kwamba wafuasi hao wa Chadema walikatazwa kwenda kwenye mkutano huo kwa njia ya maandamo na kwamba walipokaidi amri hiyo ya Jeshi hilo ndipo nguvu zilipotumika kuwatawanya.
“Nikweli kulikuwa ghasia lakini Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwatawanya na hivi sasa wamekusanyika katika eneo maalum walilopaswa kuwepo”anasema Shilogile.
0 comments:
Post a Comment