PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Efamline, Kutanua wigo kwa kuwatangaza na kuwashauri waimbaji kwa ufanisi wa huduma ya Muziki wa Kiroho na kujenga mikakati ya kiuchumi kwa kila mwimbaji.

Huduma ya Efamline ni huduma ya kujipanua kijamii na kuangaza mifumo ya Maisha na Sanaa ya Muziki wa Kiroho,ambao mwimbaji wa Muziki wa Wokovu (Salvation Music) MR. DAYOS, ameianzisha kushirikiana na watu wote kujenga utumishi wa kuwatumikia watu. kwa agizo la Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Utumishi huo ni pamoja na kuondoa uoga wa kufikiri kuwa mtu wa Mungu hapaswi kufanya Urafiki na jamii kwa kuwashirikisha maono mampya na nia mpya ya Upendo wa Mungu kwa watu wake ambao wengi wao bado hawamwamini Yesu.

Kutokana na tatizo hilo la watu kuto mwamini Mungu, watu wengi wameua uadilifu wa Imani ndani yao.
Kwanza ile hekima ya Mungu ndani yao haimo, tena hawajui Upendo wa Mungu kwao na roho zao zimejitenga na upendo wa Nungu, wengi wao wanapotea kwa mawazo ya kudhania wakifa wanapumzika.

Kuna nini cha kufikiri juu ya hawa watu? Mr.Dayos ndipo alipopata ufumbuzi wa kushukia jamii yote kwa Neno la Roho ya Mungu, kupitia Sayansi ya maendeleo na mawasiliano ya jamii, kujenga misingu ya huduma ya Ifamline.
Ambayo Inahusika na Elimu ya Mungu kwa jamii kupitia Sayansi ya Roho wa Mungu aliyeziumba Mbingu na Nchi. (Kutoka 31:1-5)  Neno hili linafungua milango ya Mbingu kuinua Hekima ya kila mtu aliyeandikiwa kujazwa hekima na Mungu, kwa kazi maalim.( 1wakorintho 12:4-11 Mungu hutoa huduma ndani ya mtu kwa kazi maalumu na wakati maalum na mahali maalum.

KWA NENO HILO NI UHALISIA WA WAZI KUWA SAYANSI KWA WATU WA MUNGU IPO.
Hivyo Ni wakati kutumia vipawa na Elimu ya Sayansi ya Mungu kuleta mabadiliko ya kwa jamii, kwa Neno na Maendeleo ya Vitu vya maisha ya kawaida.
Mfumo huu ni pamoja na kufanya huduma ya Uimbaji kwa kumtumikia watu na umoja wa kuwezeshana waimbaji tufike mbali.
Hivyo sasa kazi ya kuwatumikia watu ni pamoja na kuwapa neno kwa mifumo mbalimbali ya sayansi, maana watu wengine wanamawazo ya kuridhika na dunia, ila kupitia hii dunia na vivutio vyake,tutampa kila mtu Haki ya Mungu kadri Roho atakavyo tuongoza kutimiza agizo la kuwatumikia watu. Mathayo 28;19-20 Biblia inaonyesha maneno matatu makuu, inasema enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.

 hiki kipengele cha kwanza kwa Mr.Dayos ni Sayansi.
1.Kwenda na kuchukua hatua.
2.unawafanya kuwa wanafunzi wa Yesu.
3.Kuwafundisha kuyashika yote tuliyoagizwa kufanya kupitia neno, inamaana kama mimi nimeagizwa kufanya huduma ya maendeleo kwa jamii ya waliyookoka na wasiyookoka, huo utakuwa mfumo mpya na wakisayansi ambayo huwaunganisha watu na Mungu kupitia mazingira waliyozoea kufurahia kama vile (Ujasiliamali,Elimu,Imani,ubunifu)
Wakati mwingine mtu waweza kujiuliza kwanini nimeongelea Ubunifu, na Elimu?Nimetumia utofauti maana mtu aweza kuwa na elimu ila asiwe mbunifu.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: