PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Mchungaji DCT ajitolea kupambana na mafundisho potofu


·        Akemea  wanaotukuza kundi la Freeemason
·        Aelezea fursa sahihi za kubarikiwa na kufanikiwa
Na Joseph H. Ongong’a

Mch. Ron Swai (Chalii wa Yesu)
Mchungaji Ron Swai wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dar es Salaam Calvary Temple (DCT), amejitolea kukabiliana na kupambana  na baadhi ya  mafundisho potofu yanayotolewa  na baadhi ya watu  kupitia  njia mbalimbali ikiwemo na vyombo mbalimbali vya habari, kwa kutoa  mafundisho yatakayowatoa watu kwenye mtazamo hasi na kuwarejesha katika msingi imara wa kufahamu Neno la Mungu na kuliishia.
Ron alisema hayo hivi karibuni wakati wa ibada maalum ya jumapili kanisani kwake, ambapo alibainisha kuwa, katika nyakati hizi za mwisho, kuna kundi la watu amabao aidha kwa kutokujua Neno la Mungu kwa usahihi, ama kwa makusudi ya lazima kabisa, wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotoa maandiko na kuwahadaa watu kwa matangazo yao kuwataka wawaombee Baraka.
Ulisema yameibuka mafundisho mengi yenye falsafa potofu ambayo mtu akibarikiwa kwa wakati huu anasemwa kuwa amejiunga na Freemason, akikosa wanamwita kuombewa, ili abarikiwe, lengo ni kuwachanganya watu ili wasielewe Neno sahihi la Mungu.
Aidha Mchunga Ron Swai ailiwataka watu kuondokana na dhana hiyo potofu  badala yake walisome Neno la Mungu, kwa usahihi, waliishi na kutekeleza yote yaliyoelekezwa humo ili wapate Baraka ambazoziliahidiwa na ziko tayari kwa yule anayeamini.
Mtumishi huyo wa Mungu alisema kwamba, atahakikisha kwamba anatumia vyema madhabahu takatifu ya Mungu kuhubiri, kufundisha kwa usahihi Neno, bila kupindisha ili kubadilisha mwelekeo wa falsafa potofu iliyogandamana ndani ya mioyo ya watu wengi walioumizwa.
Mchungaji Ron alisema, ameamua kufundisha somo hilo linalohusu kanuni sahii ya kubarikiwa kwa mtu wa Mungu, baada ya kukuta na watu wengi walioumizwa na mafundisho potofu waliofika katika kanisa la DCT kuomba msaada.
Aidha Mchungaji Ron, ailiwataka watu waelewe kwamba, kabla ya vitu vyote, Freemason na  mambo mengine Mungu alikuwepo na aliisha toa ahadi kwa wamchao, kilicho salia sasa ni kuingia kwenye utekelezaji wa kumdai Mungu na sio kukimbilia ibada za maombezi ambazo mifumo yake inafanana sana na uganga wa kienyeji.
“Nasema Freemason sio kila kitu, Mungu ni zaidi ya Free mason, watu wamefikia mahali hawamchi Mungu wa kweli, badala yake wanatoa heshima na utukufu kwa vitu vusivyofaa kabisa,”  alisisitiza Ron
Mchungaji Ron,alikemea vikali tabia ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu na kutumia vibaya mimbari kuwahadaa watu kwa utabiri wao kwa lengo la kujipatia pesa. “Nasema achana kabisa  na mambo hayo, umtukuze Mungu wa kweli ili upate Baraka zake zisizo kuwa na majuto,”  alisisitiza Mchungaji Ron.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: