PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Rais Kikwete awahimiza watanzania kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa


Na Salesi Malula
RAIS Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, amewaomba Watanzania, kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa na Makazi, linalotarajiwa kuanza Leo usiku nchini kote ili wahesabiwe.
Ameyasema hayo Ikulu leo, alipokuwa anatoa hotuba yake ya Mwezi ambapo Rais hutumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari juu ya mambo yanayohusu mstakabali wa Taifa, ikiwepo kufafanua mambo mbalimbali kwa wananchi.
Katika hotuba hiyo, Rais Dk.Kikwete alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kuhesabiwa, kwani sense ni muhimu katika itaisaidia  serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.
Dk. Kikwete, amewaasa Watanzania Kupuuza uvumi wa kuipinga Sense na kusema wote wanaohamasisha watu wasihesabiwe wapuuzwe kwani, wanatumia vibaya uhuru wa kutoa maoni na hawalitakii mema Taifa.
Kamwe Serikali haiwezi kufanya sense za Kikoloni, ambapo miaka ile kabla ya nchi kupata uhuru watu waliokuwa wakihesabiwa kwa kuulizwa Dini zao na hata rangi zao maana serikali za wakati ule zilikuwa za kibaguzi mfumo ambao hauwezi kutumika kwa mfumo wa sasa ambao Tanzania iko huru.
Alisema kamwe serikali haiwezi kuchanganya mambo ya Dini na kuyaingiza serikalini kwani haifuati tena mfumo wa kibaguzi wa wakoloni hivyo wote wanaopanga kukwamisha zoezi la sense na makazi wapuuzwe na natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi ili wahesabiwe ambapo zoezi hilo linaanza leo kuanzia saa sita usiku.
Dk.Kikwete aliesema sense ya kwanza Katika taifa letu ilifanyanywa Mwaka 1910,1931,1948 na 1957 ambapo wakoloni waliokuwa wakifanya sense kwa mfumo wa kibaguzi kwa kuwauliza watu Dini na hata rangi zao.
Sensa iliyofuata ilifanyika mwaka 1967,1978,1988,202 na 2012 ambapo mwaka 1967 ilifanyika kibaguzi lakini miaka mingine mfumo ulibadilika baada ya watanzania kuwa huru rasmi.
Zoezi la Sense na makazi linatarajiwa kukamilika ndani ya siku saba japo kumekuwa na vikwazo vya hapa na pale ikiwepo baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakitaka Sensa ya mwaka huu iingize kipengele cha Dini ili wananchi waulizwe Dini wanazosali jambo ambalo haliwezekani kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kujitenga na masuala ya Dini ambapo Serikali haina Dini lakini wananchi wake hawana Dini Hivyo kuingiza kipengele cha Dini kwenye zoezi la sense na makazi itakuwa ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: