( Si kwa waimbaji tu bali kwa kila aliyemwamini Yesu)
Na Mchunganji Ency Ntepa. Mwalukasa
(LACTAN MINISTRIES)
Tunakukaribisha kuwa mmoja wa wafadhili wa huduma za uchapaji na usambazaji wa vitabu vya sifa na kuabudu.AMBAVYO VINAHITAJIKA SANA NCHINI. Mungu akubariki sana kwa utoaji wa moyo. TAFADHALI WASILIANA NASI KWA SIMU AU EMAIL ZETU TUKUPE NJIA MBADALA YA KUTUMA MCHANGO WAKO. UBARIKIWE NA MUNGU WETU.
_____________________________________________________________
UTANGULIZI
Kutokana na mapokeo na semina za kusifu na kuabudu kuwa adimu makanisani mtazamo wa waumini wengi kuhusu uimbaji wa kusifu na kuabudu ni kwamba ni huduma au uimbaji wa kupitishia muda tunaposubiri mahubiri katika ibada, semina na mikutano ya Injili au kama nyimbo tu za kujifurahisha au kama utaratibu wa kawaida ya kuimba katika Makusanyiko ya watu wa Mungu kama nyimbo zingine. Huduma hii ya kumwimbia Mungu sifa na kumwabudu imekuwa haina matunda au matokeo mazuri au yanayohitajika kiroho, kiakili na kimwili sababu ya waumini wengi kutoelewa na hatimaye kuimba bila kumaanisha au kutarajia chochote toka kwa Mungu na hatimaye mazoea na desturi kutamalaki ibada nyingi au maisha ya waliokoka. Zaidi mapokeo yametamalaki Ibada na maisha binafsi ya waumini. Wengi hawapendi kujifunza au kupokea ushauri wa mambo yajengayo kiroho au kuhusu huduma hii ya sifa zaidi waimbaji maana wanauzoefu na wamevuma. Lengo kuu la kukusanyika IBADANI ni kumshukuru ,kumsifu na kumwabudu Mungu na tukishamhudumia Mungu yeye hutuwezesha kuhudumiana kwa Neno, karama za Roho Mtakatifu kama unabii, neno la ufunuo- maarifa, uponyaji na Nyimbo za uinjilisti, kutia moyo, kufariji na kujenga. Ugonjwa mkubwa ulioko katika makanisa yetu mengi, au maisha binafsi ya waumini tumekariri mapokeo,tunapenda sana na kutoa muda zaidi katika huduma kwa watu (kuhudumiana) kwa nyimbo za kwaya zenye jumbe kwa watu kama kujitia moyo, kutiana moyo, kutamba, kuhimizana, kuhubiriana na kuwahubiria wadhambi wakati mwingine nyimbo za uinjilisti zinaimbwa kanisa la waaminio sababu tu zina muziki, melody na uchezaji wa stepu nzuri, inakuwa ni kujifurahisha tu. Ni kawaida kabisa watu kushabikia au kushangilia nyimbo za kutia moyo, kuhimizana au kuzodoa na kutamba na kukaa kama vile hatuhusiki wimbo wa sifa unapoimbwa na waimbaji wasipotuhamasisha kushiriki basi tutawatazama tu., wakati wa kumsifu na kumwabudu Mungu ndio muda wa kufunuliwa ukuu wa Mungu na nguvu zake na wema wake na nyimbo hizo ndizo zitakazoondoa tatizo lako. Nyimbo za kutia moyo zinakufariji saa ile kupitia waimbaji tatizo lako linabaki palepale, Lakini sifa zinayeyusha milima na matatizo ya maisha yako kwani ni “shortcut” njia ya mkato ya kuugusa moyo wa Mungu hata akashuka na kuwagusa watu katika matatizo yao kwa kuyaondoa au kuwaonyesha ufumbuzi au kusema nao neno la kinabii litakalowapa majibu na hatua mpya. Pia sifa humuandalia mhubiri mazingira ya upako wa kuhubiri katika Roho Mtakatifu na kutifua mioyo ya watu, na husambaratisha kila nguvu za giza na kusafisha anga na kukupa hamu au uvuvio wa kuomba kwa Mungu… hivyo ni vidokezo tu vya faida za sifa… kumiendelea kusoma kitabu hiki upate mengi.
SURA YA 1.
(i) Sifa au kusifu Mungu maana yake nini?
a)Kumsifu Mungu ni kuongea, kukiri, au kushuhudia na kuimba kuhusu Uweza wa Mungu, nguvu za Mungu, Mamlaka ,matendo makuu aliyotenda Bwana (kazi zake), miujiza, mambo ya ajabu, uumbaji na nafasi ya Mungu katika maisha yetu na uhusiano wa Mungu na wanadamu. Kwa mfano: (Mungu ni Mfalme: Wewe ni Mfalme, Baba yetu, U Bwana , Ni muumbaji wetu, ni Mchungaji, mponyaji, ni wa kwanza na wa mwisho ( Alfa na Omega) na mtoa mahitaji yetu kama majina yake yanavyomtambulisha .Una nguvu, umeumba mbingu nchi na vilivyomo, mtenda mijuza, unaweza yote, umetuponya, umetulinda, Mungu katupigania [zaburi 150:1-6]. mistari hii inaeleza tumsifu Mungu wapi, kwa nini na namna gani au kwa kutumia nini.
b)Pia sifa ni namna mojawapo ya kujitoa sisi wenyewe kwa Mungu kama sadaka (dhabihu za sifa), ni kumuenzi na kumkubali, Mungu ni nani na aliyoyatenda kwa mioyo yetu, nafsi , akili, nguvu na miili yetu yote inatakiwa ihusike. [Waebrania 13:15] “Basi kwa njia yake yeye na tumpe Mungu dhabihu za sifa daima yaani tunda la midomo liungamalo jina lake .
[Warumi 12:1-2] “Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu yenye kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”.
Imefika kipindi cha sasa tunatakiwa tuache kuahidi kumsifu Mungu kama Daudi aliposema “nitakutukuza, nitamwimbia Bwana, kwani alikuwa katika vita na kutangatanga porini akimkimbia Sauli hivyo alikuwa akiahidi kumsifu Mungu atakapookoka . Sifa zenye mguso kwa Mungu ni zenye maneno ya kumwambia Mungu moja kwa moja kama vile unamuona au unaamini yupo hapo unapoimba au kutamka sifa zake...”Ninakuimbia Bwana, ninakusifu mfalme..
Ni maombi yangu kwamba kitabu hiki kitakutoa katika, desturi za ibada, mapokeo ya kipentecost au liturgia na udini uliowafunga wakristo wengi, kitabu hiki kikusaidaie kupata uamusho wa kiroho na kuifanya huduma ya kusifu na kuabudu kuwa sehemu au mtindo wa maishayako ya kila siku. Kwani kusifu na kuabudu ni mahali popote, wakati wowote na hata ukiwa peke yako. “ Mfalme Daudi alisema [ zaburi 146:1-2] Nitamsifu Mungu ningali hai, muda ninaoishi.” Aliamua kumsifu Mungu asubuhi, mchana na usiku mara saba kwa siku. Akapewa jina la “mtu autafutaye moyo wa Mungu”
Kumbuka huduma zote zitakoma hapa duniani isipokuwa kusifu na kuabudu kutaendelea mbinguni milele na milele lazima uipende na kuanza kuifanyia mazoezi huduma ya sifa na kuabudu kwa kuienzi na kutoa muda zaidi. Kwani ibilisi anaipiga vita huduma ya sifa na kuabudu anajua ni kiboko kwake ndio maana amewafunga waumini wengi wasiienzi .
(ii) Kwa nini tunamsifu Mungu Kupambanua nyimbo za sifa na zisizo za sifa
1.Tunamsifu Mungu kwa sababu anastahili kupewa sifa kwa jinsi alivyo, anayoyatenda, nguvu zake, nafasi yake,uumbaji au kazi za mikono yake na majina yake . Pia malaika, wenye uhai wanne na wazee ishirini na nne walioko mbinguni wanakiri hivyo [ufunuo 4.11 “Umestahili wewe Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu, hesima na uweza, kwa kuwa wewe ndiye uliyeviumba vitu vyote….”
2.Kwa sababu Mungu hupenda kukaa (huketi) katika sifa za watu wake Israel (walioamini) [zaburi 22:3] “ Na wewe umtakatifu uketiye juu ya sifa za Israel”.
3. Ni njia moja ya kumtambua, kumkubali na kumweleza Mungu jinsi tunavyomjua, au kumuona au kusikia au kusoma habari zake katika Neno la Mungu hatimaye tunamuenzi atamalaki maisha yetu au katika Ibada amiliki na kuongoza yeye.
4.Kama waumini tumeitwa kumsifu na kumwabudu yeye .[1Petro 2:9] “ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake (yaani sifa zake biblia ya kingereza inasema) yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.
5.Ili kuwajulisha maadui zetu (shetani) ukuu, uweza na nguvu za Mungu wetu, hii husababisha Imani zetu kukua na kuongezeka na hatimaye majaribu na matatizo tunayokumbana nayo katika maisha kupungua au kuyeyuka na Mungu wetu kuwa mkuu na ndipo tunaona ushindi wa Bwana.
· Unavyozidi kumtukuza Mungu wako ndivyo Mungu huwa karibu nawe na kuwa Mkubwa zaidi, na shetani huwa mdogo na kukimbia kuwa mbali nawe.
6.Sababu kusifu ni Amri kwa kila kiumbe sio uchaguzi au kujisikia. [zaburi 150:6] “ Kila mwenye pumzi amsifu Bwana , Haleluya”.
· Hapa tunapata changamoto ya kuifanya huduma ya kumsifu Mungu mtindo wa maisha yako binafsi yaani wakati wote sio hadi uwe ibadani ,fellowship au katika semina tu.
(iii) Jinsi ya kutambua nyimbo za sifa na zisizo za sifa na namna ya kutunga wimbo mpya.
Ni vema kama wewe kiongozi wa sifa uwe na orodha ya nyimbo au pambio nitakozozianisha hapo chini kwa makundi ya aina za ujumbe wa sifa. Sio kuimba pambio zile zile ulizosikia au ulizozowea na ndio maana hazikugusi wala kumgusa Mungu sababu umezizowea na hujiachiia kwa Roho Mtakatifu autengeneze uwe mpya ( ahuishe wimbo) sababu huna muda wa maandalizi binafsi ukautafuna wimbo ukawa wako na kukuunganisha na Mungu. Neno linasema “mwimbieni Bwana wimbo mpya”. Unaweza ukatunga wimbo kila siku ukipania na kumsikiliza Roho Mtakatifu.Unapoabudu katika Roho Mtakatifu hukuletea sauti ‘melody’ nzuri katika lugha na baadaye unaweza weka maneno ya lugha yako. Nilipokuwa kiongozi wa sifa kila wiki nilitunga pambio jipya au Roho Mtakatifu alinikumbusha, pambio za nchi zingine au za zamani nikazitengeneza kwa upya (kuzimodify)na za makabila mengine nikazitafsiri, sawa na ujumbe wa wiki kama uweza au kuinua, shukrani, upendo wa Mungu na pambio hilo likanishushia uwepo wa Mungu na hata wanakikundi cha sifa likawabariki katika mazoezi yetu na kuwagusa washirika katika ibada na uwepo wa Mungu kushuka kwa nguvu isivyokawaida.
Angalizo: Ewe kiongozi wa sifa, au muimbishaji si kila wimbo au pambio lenye mdundo wa haraka unaochezeka ni sifa lazima uwe na meneno yenye maana niliyotoa kuhusu sifa ni nini. Mfano: Ameniona x10 wanarudiarudia sio sifa , Nimeamua sitarudi nyuma, Naimbaimba sababu nimeokoka ,“ Nimeamua ooh sitarudi nyuma hata iweje..”Mnara wa babel lazima uanguke,mifano ya nyimbo hizo sio sifa ni ushuhuda na kujitia moyo na kujihurumia. Unakuta tunapoteza muda katika ibada na Mungu hadhihiriki sababu tunajifariji na kutiana mioyo na kutambiana badala ya kumhudumia Mungu kwa kumsifu yeye. Au “ Yende mbele Injili wee yende mbele, sio SIFAAA. Huo ni wimbo wa mkutano wa Injili. Sikuachi usiponibariki eeeh.
Muimbishaji wa sifa uwe na ufahamu wa kiroho, ULIJUE neno linavyomwelezea Mungu katika Zaburi, ufunuo, Isaya, Ezekiel n.k. umjue Mungu ili unapoimbisha umpambe na kumwelezea Mungu kwa wasifu wake, tabia , uweza ,matendo ili wanaoitikia au kusikiliza wafunuliwe na kumjua huyu Mungu ndipo Mungu anawagusa, sio unaimbisha maneno yale yale uliyosikia katika hilo pambio likiimbwa huna ubunifu wowote wala kuzama kufunuliwa na Roho Mtakatifu. Usitegemee mguso wa Mungu kwako wala unaowaombisha. Japokuwa mara nyingine Mungu hushuka kwa neema anatuchukulia sawa na upeo wetu kuna wakati utagota kuimba nyimbo zilizozoeleka.
Light And Comfort To All Nations
P.O.BOX 78091
DAR E SALAAM, TANZANIA
TEL: : +255-759 228282 / +255-715 672748
0 comments:
Post a Comment