Na Mwandishi wetu-Manyoni
Wananchi wa maeneo ya Majengo,na Kipondoda wilayani Manyoni
Mkoani Singida wanatarajia kufanya maandamano makubwa kupinga hatua ya uongozi
wa wilaya kuwanyang’anya maeneo yao na kuyauza kwa watu wengine huku wenye
maeneo wakiachwa bila kupewa fidia yeyote.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni na baadhi ya Wananchi |
Mwenyekiti anayeratibu
maandamano hayo Bw.Ufinyu cheliga akiongea katka mahojina maalum alisema
wanatarajia kufanya maandamano makubwa ya Amani kupinga kunyang’anywa maeneo
yao ambayo wanayamiliki kihalali na wanatarajia kuwakilisha kilio chao hicho
kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Alisema watampa kero zao na kumuomba awatimue kazi mkurugenzi
wa wilaya,Afisa Ardhi na mwenyekiti wa
Halmashauri kwa sababu hawa ndio tatizo kwenye mgogoro huu wa masuala ya Ardhi
kwani wamejigawia maeneo mengi na wameshindwa kuwafidia wananchi wanaomiliki
maeneo hayo.
Alipoulizwa ni kwa nini wapeleke kero kwa mkuu wa Mkoa wakati
mkuu wa wilaya yupo.Bw.ufinyu alisema katika kikao chao na wananchi wamekosa
imani na mkuu wa wilaya kwani wakati wa kujitambulisha walimkabidhi kero
mbalimbali lakini mpaka hivi leo hakuna hata kero moja ambayo ameshaifanyia
kazi hivyo “tunaona itakua ni mambo yale yale tu bora tumpe kero mkuu wa mkoa
aweze kulishughulikia”.Fatma yaufiki.fotunata marya
Mkurugenzi wa wilaya ya manyoni Bi.Fotunata Marya
alipotafutwa kwa simu yake ya 0784
224933 kujibu tuhuma za kutumia mamlaka yake vibaya kwa kujimilikisha viwanja
simu iliita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi kujibu tuhuma ambazo
wananchi wanamtuhumu hakuweza kujibu.
Naye mkuu wa Wilaya ya manyoni Bi.Fatma Toufiq akiongea
katika mahojiano maalum alikiri kuwepo kwa migogoro ya Ardhi na tayari kero
zote zimeshafika mezani kwake anazishughulikia na kuhakikisha anazimaliza.
Alipoelezwa juu ya kero ambazo wananchi wamempa na ameshindwa
kuzitekeleza Bi fatma alisema “kero ambazo wamenipa ni nyingi wao hawaoni
karibu kero nyingi ambazo wamenipa nimezitekeleza hivyo si kweli kwamba mimi
nimepuuza bali naendelea kutatua kero moja baada ya nyingine na kuhusu suala la
maandamano itakua si busara kwani tayari mambo wanayoyalalamikia wananchi
nayafanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment