PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

UCHAGUZI MKUU WA MAJIMBO YA TAG


UCHAGUZI  WA  MAJIMBO
Jimbo la Mashariki Kusini  yawa kielelezo
·         Viongozi wake wote wapiti kwenye kura za maoni
·         Sehemu(Section) zake nazo zaongoza.
·         Askofu Kametta awaomba mshikamano.
Katika uchaguzi wa majimbo 23 kati ya 25 ya kanisa la TAG, yaliyopiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Dodoma, hivi karibuni, Jimbo la Mashariki limetia fora klatika kuwachagua  Viongozi wake, baada ya kuwapitisha wote  kwenye kura za wali za maoni.
 Aliyeongoza kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi ni aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Dk. Lawrence Kametta aliyepita moja kwa moja  kwenye uchaguzi wa kupendekeza majina yanayostahili kupigiwa kuara.
Askofu Dk. Lawrence Kametta, alipita  baada ya kupata theluthi mbili za  wapiga kura wote na kutangazwa  moja kwa moja na msimamizi wa uchaguzi huo Mwalimu Geoge James , kuwa Askofu mpya wa Jimbo hilo kwa awamu nyingine ya  miaka minne ijayo.
Msafara wa baadhi ya wachungaji na Maaskofu wa Kanisa la TAG, wakielekea kwenye kumbi za Chuo Kikuu cha UDOM, walipoelekezwa kwenda kuwachagua maaskofu wa majimbo na viongozi wao wa Sehemu. Picha na Joseph Ongong'a
Viongozi wengine wa Jimbo hilo waliopitia moja kwa moja kwenye kura za maoni ni pamoja na Makamu Askofu, Mchungaji Eliya Lugwami, katibu wake Mchungaji Emaniel Mziray  ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa katibu wa jimbo hilo, Mchungaji Charles Luoga, aliyeomba kuondolewa jina kwa sababu ya masomo.
Wakati Jimbo la Mashariki ikitia for a kwenye uchaguzi huo kwenye nafasi za sehemu na jimbo,  kwenye majimbo mengine hali ilikuwa ya vuta nikuvute baada ya kutokea upinzani mkali kati ya wagombea  jambo lililopelekea kurudiarudia kupiga kura.
Majimbo ambayo yalionekana kuwa na upinzani mkali ni pamoja na   Arusha,  Mbeya  na Singida, ambapo kazi ya kuwapata Viongozi katika majimbo hayo na mengi haikuwa  rahisi sana kama ilivyokuwa kwa Jimbo la mashariki kusini.


 Wachungaji walioko Jimbo la Mashariki Kaskazini na Viongozi wao waliomaliza muda wao wakisubiri kupiga kura wakati wa uchaguzi Mkuu uliofanyika UDOM, hivi karibuni. Hata hivvyo Viongozi wote wa zamani walichaguliwa na kuendelea na nafasi zao


Aidha Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo hilo mara tu baada ya kumalizika kwa kazi ya uchaguzi, aliwapongeza Wachungaji hao kwa moyo wa utulivu walio nao na kuwa na imani na vyongozi wao.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa Majimbo yote, katibu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Mchungaji Ron Swai, alisema kuwa, jumla ya maaskofu wanane na wasaidizi wao 14 wamekosa nafasi ya kuendelea katika nafasi zao.

Baadhi ya Maaskofu, na wasaidizi wao wakiwa katika picha ya pamoja
Jimbo lingine ambalo limewarudisha viongozi wake wote waliokuwepo awali ni lile la Mashariki Kaskazini ambapo Askofu Geoffrey Massawe,   alichaguliwa  tena kuwa Askofu wa Jimbo hilo kwa miaka minne mingine ijayo, pamoja na makamu wake Mchungaji Spear Mwaipopo na katibu wao Mchungaji Charles shila naye amerudia kwenye kiti chake.
Akiongea  mara tu baada kuchguliwa tena kwenye jimbo lake, Askofu wa Jimbo la Mashariki na Kusini,   

 Dk. Lawrence Kametta,  ailiwataka wachungaji wote wa makanisa yaliyoko katika jimbo hilo kuwa na ushirikiano katika utendaji wao wa kazi.
Aidha alisema kuwa, bila ushirikiano katika jambo lolote lile uongozi unaweza kuwa na kazi ngumu sana, na kwamba hakuna mafanikio kwenye utengano.



Hata kama kura imetupambanisha lakini bado tuna upendano wa Kristo. "Tuwe na mshikamano katika kutekeleza kazi ya Mungu"
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: