Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dk. Barnabas Mtokambali, akimkabidhi kiti maalum cha kubembea Mhubiri Maury Davis, kutoka Marekani wakati walipokuwa wakiagana naye katika ukumbi wa Chimwaga ulipofanyika Mkutano Mkuu wa kanisa hilo jijini Dodoma. Pamoja na zawadi hiyo Askofu Dk.Mtokambali alimkabidhi Mhubiri huyo Bendera ya Tanzania kama ishara ya kuonesha ushirikiano na mshikamano wa nchi ya Tanzania na USA. Kushoto ni Makamu Askofu wa Jimbo la Dodoma, Mchungaji Wilberforce Mongi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Dk. Barnabas Mtokambali, kulia wakifanya maombi maalum kwa Rev. Maury Davis, wakiwa wameshikilia Bendera ya Tanzania. Kushoto ni Makamu Askofu wa kanisa hilo, Dk. Magnus Mhiche.
Wamama Viongozi wa Kanisa la TAG taifa, (nyuma), wakiwa katika picha ya pamoja na Mmisionari anayemaliza muda wake nchini Tanzania, Ron Hansen na mke wake, waliovalia mavazi ya asili ya kiafrika. Askofu Dk. Mtokambali na kamati yake walimkabidhi mmisionari huyo na mke wake zawadi nyingi sana kwa ajili yake na familia yake. Baadhi ya maaskofu waliomaliza muda wao katika kanisa la TAG, walitoa shukrani zao kwa wamisionari hao, kiasi cha kuwaliza. (Picha zote na Joseph Herman Ongong'a)
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment