Waislamu wavamia mahakama kutaka kumua mtoto aliyekojolea msaafu.
Na Joseph. H Ongong'a
Kundi la waislamu wenye itikadi kali za kidini
limevamia kituo cha polisi Mbagala Kizuiani kutaka kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 10,
kwa madai ya kukojolea msaafu. Katika tukio hilo, kundi hilo lilivamia kanisa la Tanzania Assemblies of God Mbagala Kizuiani na kurusha mawe na kusababisha hasara mbalimbali na pia baadhi ya magari yalivunjwa
vioo na barabara kufungwa, jambo lililolilazimisha Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya . Hata hivyo
kamanda Kova kutoka na tukio hilo alisema kuwa tukio hilo lisichukuliwe uzito
wowote, kwa vile ni la kitoto na halikuwa na kusudi lolote. Inadaiwa mtoto huyo na rafiki yake walikuwa wanabishana na ndipo tukio hilo likatokea, baadae wazazi wao baada ya kufikishiwa tukio hilo la kukojolea kitabu hicho walikaa na kukubaliana kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya makubaliano yao na ndipo kundi la waislamu wakajitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kumtaka mtoto huyo wamuue.
0 comments:
Post a Comment