PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

UCHAGUZI MKUU TAG


Askofu Dk. Mtokambali achaguliwa tena kuongoza TAG
·        Aibuka na ushindi wa theluthi mbili ya kura zote
·        Arudi madarakani  na timu yake yote 

Na Joseph Herman 

Katikati ni Askofu Mkuu wa TAG, Dk. Barnabas Mtokambali akiwa katika picha ya pamoja na timu yake mara baada ya kutangazwa washindi. Kulia kwake ni Makamu wake Askofu Dk. Magnus Mhiche na Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Mchungaji Ron Swai. (Picha na Joseph Ongong'a)
Askofu Dk. Barnabas Mtokambali akifuta machozi mara baada ya kutangazwa mshindi

Katibu Mkuu wa TAG Ron Swai aliyeshika kichwa akinyamazishwa ma Mchungaji Kimaro
Kwa mara nyingine tena Askofu Dk. Barnabas Mtokambali wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne mingine ijayo baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga ulioko katika Chuo cha UDOM, mjini Dodoma wiki iliyopita.

Akitangaza matokeo hayo Mmisionari Gregorry Beggs, kutoka USA, alimtangaza Askofu Dk. Mtokambali kuwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo kwa awamu nyingine  baada ya kupata theluthi mbli ya kura zote zilizopigwa wakati wa mapendekezo ya majina ya wagombea, ambapo idadi ya wapiga kura wote waliokuwa ni 2717, na Dk. Mtokambali alipata kura 1969, kati ya kura 2116 zilizopigwa sawa na asilimia 93.

Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri kuu wakiwa katika ukumbi wa Mkutano mjini Dodoma
Aidha alisema, kulingana na katiba ya kanisa la TAG, linaruhusu kumtangaza mshindi endapo atakuwa amepata theluthi mbili za kura zote zilizopigwa wakati wa mapendekezo ya majina ya wagombea.

Katika uchaguzi huo Mmisionari Berggs alimtangaza Askofu Dk. Magnus Mhiche, aliyeshinda nafasi ya umakamu Askofu Mkuu wa kanisa hilo kwa mara nyingine tena, baada ya kupata kura 1009 kati ya kura 2019, zilizopigwa.
Kushoto ni Makamu Askofu Mkuu wa kanisa la TAG aliyemaliza muda wake miaka ya nyuma, aliyemwachia Dk. Mtokambali kijiti, Dk. Rogathe Swai, akiteta jambo na Mtokambali muda mfupi kabla ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Dodoma. (Picha na Joseph Herman Ongong'a).

Katika nafasi ya Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Mchungaji Ron Swai naye ameibuka kidedea na kurudia tena katika nafasi yake, ya ukatibu baada ya kupata jumla ya kura 1878 kati ya kura 1979, zilizopigwa.

Sehemu ya wajumbe wa Mkuatano Mkuu wa TAG, waliohudhuria wakiwa ukumbini
Kwa matokeo hayo,  inampa nafasi Dk. Barnabas Mtokambali na timu yake yote kuongoza tena kanisa la TAG, kwa awamu nyingine ya miaka minne ijayo baada ya kuongoza kwa miongo ya miaka minne iliyopita.

Uchaguzi mwingine unaotarijiwa kufanyika ni ule wa Viongozi wa Majimbo na Sehemu.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: