PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Mchungaji Azindua Operation maalum ya wiki tano ya maombezi na uponyaji


Ø Asema sasa ameamua kutangaza mpango kabambe wa kuwafungua watu
Ø Asema  kuna kikundi cha wahuni kimejipenyeza  kuadaa ulimwengu
Ø Waliodanganywa na kupewa vitambaa, vyungu,  mafuta wavisalimisha


 Joseph ongonga na Salesi Malula

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre, la Majumbasita Ukonga Jijijini Dar es salaam,  Moses Magembe, amezindua kampeni maalumu ya maombi na maombezi, kwa muda wa majuma matano, ambapo kazi ya kuwafungua na uponyaji unaoambatana na matendo makuu ya nguvu za Mungu  utaanza rasmi.
Akiongea katika Ibada ya  hiyo maalum alisema  kazi ambayo ameianza haitazimwa bali ameamua kuwasha moto katika siku za Jumatano,Alhamisi,Ijumaa na Jumapili kwa muda wa majuma yote matano fulululizo, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na Vitongoji vyake, wakiwepo watu kutoka mikoa mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maombezi hayo muhimu kwani katika kanisa hilo, masuala ya miujiza siyo kitu cha kushangaza bali watu wamekuwa wakitendewa na Mungu pasipo shaka.
Akitoa mfano alianza kwakuwainua makundi mbalimbali  ya watu ambao wametendewa miujiza na walioponywa ukimwi na kuthibitishwa na madaktari ,wakifuatiwa na kundi lingine la watu waliokuwa wakiteswa na vifafa, waliokuwa hawapati watoto na wale ambao wamebarikiwa Baraka mbalimbali, zikiwepo kujenga nyumba,mashamba,magari n.k, mkundi yote hayo yaliweza kusimama na kudhihirisha kuwa hakika Mungu amewatendea.
Huku akisimamia somo lake la Jina la Yesu ni jina la Pekee, huku akikemea mfumo wa kanisa kugeuka kuwa kibanda cha Waganga wa kienyeji kwa kutumia mifumo ya kuwapaka watu mafuta na wengine kuyauza kwa gaharama kubwa, jambo ambalo alisema kuwa ni upotofu wa hali ya juu wa kiimani, kwani jina la Yesu halihitaji msaada kwani msaada ni Roho mtakatifu pekee na si njia za ujanja ujanja za unaofanywa na waganga wa kienyeji.
Akiongea kwa upako wa aina yake uliojaa nguvu za Mungu, Mchungaji Magembe alisema Jina la Yesu, halijafilisika kiasi cha kuhitaji msaada wa mafuta,chungu,fruto, wala kibakuli kwani jina hilo limemwaga damu mara moja na linauwezo wa kuwaweka watu huru pasipo mazingaombwe yoyote.
Kinachotakiwa madhabahuni ni Biblia tu, na wala sio ujanja wa kugeuza Black Curent, eti damu  ya Yesu, ambao alisema kuwa  huo ni ujanja wala sio kweli kwani, watu wamefundishwa vibaya na wamekuwa wakielekezwa kama waganga wa kienyeji wanavyofanya kwa wateja wao kwa kuwalazimisha watu kutembea na mafuta,chumvi,na makorokoro mengine.
Katika ibada hiyo ya kipekee, Mchungaji Magembe alifundisha na kuwaelekeza watu kweli ya Mungu, ambapo watu wengi walikuwa wamesalimisha vitambaa,chumvi,mafuta,chungu,shanga na makolokolo mengine ambayo walikuwa wamepewa na wahubiri yakiwepo maua ya Baraka.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign, Majumbasita Ukonga, jijini Dar es Salaam na Mchungaji msaidizi wa Kanisa hilo, Hilda Magembe wakiwa Ibadani.( Picha Zote na J&M WAMOJA BLOG)
Wafanyakazi wa Wapo Radio nao walikuwepo kwenye mkakati huo maalum
Watu wengi walifunguliwa kupitia Ibada hiyo ya kipekee mara baada ya kuombewa na mpakwa mafuta wa huyo wa Bwana, Mchungaji Moses Magembe ambaye ameamua kujitoa mhanga, kuieleza kweli mbele ya jamii ya Wakristo, na kuipinga imani potofu zilizozagaa nchini, huku akiamua kuendesha Operation maalumu, ya maombezi kupitia jina kuu la BWANA Yesu Kristo.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: