· Makarani watangatanga mitaani ovyo washindwa pa kuanzia
· Wengine wakutwa katika vibanda vya kuuza vitumbua, maandazi na baa
· Wagoma kupigwa picha na kuigeuzia kamera mgongo
Joseph Ongong’a na Salesi Malula
ASUBUHI ya siku ya kwanza ya zoezi la Sensa na Makazi linalokusudia kuwahesabu Watanzania ili kupata takwimu sahihi itakayoifanya Serikali ya Tanzania ,kupanga mipango na maendeleo yake endelevu kwa usahihi, zoezi hilo limeanza kwa kusua sua na kuonekana halijapangiliwa vyema kama ilivyokusudiwa kiasi kwamba, makarani wengi walionekana kutojua mwelekeo wao na nini chakufanya kwa ufanisi, ambapo wengi wao walikutwa wakizubaa katika maeneo ya vibanda vya wauza maandazi, vitumbua mabaa na magenge ya matunda, wakitafuta watu wa kuwahesabu pasipo mafanikio.
Waandishi wa Mtandao wa Blog ya “J&M WAMOJA” umefanya utafiti katika maeneo ya Wilaya ya Temeke, na vitongoji vyake, ambapo walishuhudia makarani wa Sensa hiyo muhimu kwa taifa la Tanzania, wakizurura ovyo mitaani kiasi kwamba walikuwa wanaonekana hawajui mahali pa kuanzia, jambo ambalo kama halitarekebishwa mapema wakati wa zoezi hili, halitaweza kufanikiwa kupata takwimu sahihi itakayo saidia Serikali katika kupanga mipango yake.
Wamoja imeshuhudia makarani hao wakiendesha zoezi hilo, katika vibanda vya wauza maandazi,mamalishe,na kwenye baa, jambo ambalo lilionekana Mabalozi wa nyumba kumi, ambao wanayajua makazi ya watu kwa karibu sana kutoshirikishwa ipasavyo katika zoezi hilo, muhimu na kuwapa kazi ngumu makarani wengi ambao wameonekana wakizurura ovyo, huku wakiwa hawajui waanzie wapi.
Mpaka majira ya saa nne asubuhi, makarani wengi katika maeneo ya Mbagala Charambe,Rangitatu,Temeke na Tandika na Vetinari, waliokuwa wanahaha na kuzunguka ovyo pasipokuanza zoezi, huku wakiwa wamebeba makbrasha yao mikononi.
Kamera ya mtandao wa J&M WAMOJA, ilimnasa Karani mmoja akiwa amevamia eneo la wauza mandazi na kuendelea na jukumu lake la kuandikisha, huku mamalishe wakiendelea na kazi ya kusukuma chapatti i, kwaajili ya maandalizi kwa wateja wake bila kuwajali na wengine wakiwakimbia na kukwepa kupigwa picha.
Ilipotaka kupiga picha Karani huyo alikuja juu akiohoji kwa nini amepigwa picha na hii ni kutokana na uelewa mdogo wa karani huyo katika medani ya masuala ya Habari.
Zoezi hili endapo litaendelea hivi litaaleta Idadi kubwa tofauti na malengo ya Serikali, kwani mfumo wa kuwafanyia sensa watu kwenye baa,na vibanda vya mama lishe, hauwezi kufanikiwa kwani uwezekano wa mtu yule yule kuhesabi wa mara mbili ni mkubwa, kwani kwa sababu ya makarani kutopangiliwa huku wakifanyakazi kwa mfumo holela, uko uwezekano kwa karani mwingine kwenda kwenye nyumba ya muuza maandazi au zile za kupanga na kuwahesabu tena.
Ili ufanisi uweze kufanikiwa ni vyema wananchi wakahesabiwa katika makazi yao na siyo kwenye vibanda vya mamalishe na kwenye baa ambapo Mabalozi wa nyumba kumi ni watu muhimu sana katika kufanikisha zoezi hilo muhimu, kwani wao ndio wanazijua nyumba zote wanazotawala na wakitumiwa vyema zoezi litafanikiwa chakusikitisha kila karani alikuwa anajiendea ovyo na hata mabalozi wa nyumba kumi inaonekana hawakushirikishwa vyema.
Wakati huo huo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre la Majumbasita Mchungaji Moses Magembe, wakati wa ibada ya jumapili ya kuanza kwa zoezi hilo, aliwahimiza waumini wa kanisa lake analochunga, kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la sensa kwa kuitikia wito wa Serikali ambapo suala la Sensa ni la Kibiblia.
Akionyesha kusikitishwa na watu wanaohamasisha wengine wasihesabiwe amesema hao watakuwa ni watu wa ajabu sana kwani watakuwa hawalitakii mema taifa hili kwani sensa ni jambo la muhimu na ni la Kibiblia, kwakuwa hata Yesu na wazazi wake walilitekeleza.
0 comments:
Post a Comment