Dk Barnabas Mtokambali arejea tena kuionoza TAG na timu yake yote.
ASKOFU MPYA WA TAG 2016, DK BARNABAS MTOKAMBALI(KUSHOTO) AKITETA JAMBO NA BADHI YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA KANISA HILO. MKUTANO HUO ULIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA CHIMWAGA ULIOKO UDOM, DODOMA
DK. MTOKAMBALI AKIWA CHINI ARDHINI AKIWASHUKURU WAJUMBE WA MKUTANO HUO KWA KUTOA USHIRIKIANO NAO KWA MIAKA YOTE MINNE WALIPOKUWA KWENYE UONGOZI KUANZIA 2012 HADI 2016
Askofu Dk Barnabas Mtokambli, amechaguliwa kwa awamu nyingine tena kuongoza kanisa hilo, kwa miaka minne. Dk. Mtokambali aliibuka mshindi katika kura za maoni kwa kupata jumla ya kura 2250, kati ya kura 2403 zilizopigwa, akifuatiwa na askofu Lawrence kametta aliyepata kura 128.
Ushindi huo wa 2/3 sawa na asilimia 75 ya kura zote, ulimfanya msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Mmishenari Gregory Beggs kumtangaza Dk. Mtokambali kuwa Askofu mkuu kwa awamu hiyo ya tano.
Mkutano huo pia ulifanya uchaguzi kwa upande wa makanu, ambapo askofu Dk.agnus Mhiche naye kwa mara nyingine ya tatu amechaguliwa kuwa makamu askofu Mkuu, baada ya vuta nikuvute kati ya Askofu Lawrence kametta, iliyosababisha uchaguzi kurudiwa mara tatu mfululizo.
Kwa ufande wa katibu, Mchungaji Ron Swai naye amerejea kwenye nafasi yake baada ya kuteuliwa na wapinzani wawili na kuwabwaga kwenye kura za awali na kutangazwa kuwa katibu mkuu kwa awamu nyingine tena.
Kuchaguliwa kwa viongozi hao imewarejesha wote waliokuwepo kwenye nafasi hizo bila kufanyika mabadiliko yoyote. Hata hivyo katika mkutano huo ulifanyika uchaguzi wa viongozi waajimbo, sehemu na kamati zao.
AKOFU DK. KAMETA AKIPIGA KURA WAKATI WA MKUTANO HUO MKUU.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment