Gazeti la Marca limeripoti kwamba, Gareth Bale amesaini mkataba wa
miaka mitano kuendelea kuitumikia Real Madrid, hiyo inamaanisha Bale
anamkataba na Madrid hadi mwaka 2021.
Cristiano Ronaldo alikubali kusaini mkata mpya mpya na Real Madrid ambao unatarajiwa kuwekwa wazi mapema mwezi September.
Mkataba mpya wa Bale utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa kitita
kikubwa cha pesa ndani ya Bernabeu, atakuwa akichukua euro milioni 10
kwa msimu sawa na nahodha Sergio Ramos huku wakiwa nyuma ya Cristiano
Ronaldo.
Nyota huyo wa Wales alikuwa na kiwango kizuri wakati wa michuano ya
Euro 2016 na kuisadia timu yake kufika hatua ya nusu fainali ya michuano
hiyo huku akianza vizuri pia msimu wa La Liga kwa kufunga magoli mawili
ugenini dhidi ya Real Sociedad.
Real Madrid imefanya usajili kwa wachezaji wachache katika dirisha la
majira ya haya ya joto barani Ulaya, licha ya kumrejesha nyumbani
Alvaro Morata kutoka Juventus baada ya kuwa katika kiwango kizuri katika
Serie A.
Kwa Florentino Perez kipindi hiki kimekuwa cha kawaida ambapo rais
huyo wa Madrid hajaangalia jina kubwa katika usajili licha ya mwanzoni
kuhusishwa na Paul Pogba.
Inaonekana Madrid imejikita katika kuhakikisha wachezaji wake wenye majina makubwa hawatoki katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment