Mkutano
Mkuu wa dharura wa CUF umevunjika baada ya kundi la wafuasi wa chama
hicho kuvamia na kufanikiwa kuzima mchakato wa kupiga kura kumchagua
mwenyekiti mpya, wakishinikiza Profesa Ibrahim Lipumba aruhusiwe kurejea
katika wadhifa huo.
Wafuasi hao wameingia ukumbini wakati
wajumbe zaidi ya 700 wa mkutano huo wakijiandaa kupiga kura kumchagua
mwenyekiti, jambo lililozua vurugu zilizoambatana na uvunjaji wa viti na
meza.Kufuatia hali hiyo, mwenyekiti wa mkutano huo, Julius Mtatiro amelazimika kuahirisha uchaguzi mpaka utakapotangazwa tena.
Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu
wadhifa huo Agosti, mwaka jana baada ya kutofautiana na vyama
vinavyounda Ukawa kwa kumpokea Edward Lowassa, alitoka nje ya ukumbi wa
Blue Pearl ulikofanyika mkutano huo, huku akisindikizwa na vijana
waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu.
0 comments:
Post a Comment