MWANASIASA
maarufu nchini Kenya, Raila Odinga, amesema amemuuliza Rais John
Magufuli kuhusu hatua yake ya kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani
hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Odinga ambaye anaongoza muungano wa
vyama vya upinzani nchini Kenya (CORD), alisema tofauti na maelezo
anayoyasikia nje, katika mazungumzo yao Rais Magufuli alimwambia
hajapiga marufuku mikutano ya kisiasa ikiwemo ile ya wanasiasa au
viongozi wa juu wa kitaifa wa vyama vya siasa wasio na majimbo.Alisema
badala yake alimwambia amepiga marufuku mikutano ya kubeba watu kwenye
mabasi kutoka eneo moja kwenda jingine kwa madhumuni ya kufanya vurugu.
“Jana mimi nimeongea na Rais yeye
ameniclaim tofauti okey…amesema hajawanyamazisha wasiongee, anasema
wanataka kufanya maandamano katika jimbo zile zingine ambazo hawana watu
na kutaka kubeba watu kwa mabasi yeye alisema wakitaka hivyo wafanye
kwao na si kubeba watu kutoka eneo hili kwenda eneo lingine, sasa sijui
ukweli mimi maana mimi si Mtanzania.
Alipoulizwa kama pengine Rais Magufuli
amemweleza msimamo wake wa kupiga marufuku siasa za ushindani hadi mwaka
2020 pia ulilenga kuwazuia viongozi wakiwemo wale wa juu wa kitaifa wa
vyama vya upinzani wasio na majimbo, Odinga alisema huku akimalizia na
kicheko;
“Anasema hajakataa.”
UKAWA WALIKOSEA KUSUSIA BUNGE
Akielezea mtazamo wake kuhusu uamuzi wa
wabunge wa vyama vya upinzani wanaounda Ukawa kususia vikao wa Bunge
kwa hoja ya kudai kunyimwa haki na kukandamizwa kidemokrasia, Odinga
alisema uamuzi huo ni makosa makubwa kufanywa na wapinzani.
“Nafikiri ni makosa sana kususia Bunge,
Bunge ni platform ambayo wapinzani wako nayo ya ku – engage Serikali,
hapo ndio wewe unaweza ukasimama ukatoa maoni yako na maoni ya watu
ambao unawawakilisha.”
AMTAKA LOWASSA AJIFUNZE KUTOKA KWAKE
Katika mahojiano hayo, Odinga
alipoulizwa alichojifunza katika harakati za kisiasa za Lowassa na hatua
yake ya kuhamia upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, alisema
mwanasiasa huyo ni mwanafunzi kwake na akamtaka aende kujifunza.
Katika hilo, alisema: “Sio mimi nijifundishe, Lowassa ndiye anayeweza kujifundisha kwenye siasa zangu.
“Ndio anaanza sasa ni mwanafunzi
anaweza kuja kwenye shule yangu (anacheka) tayari kujua yale ya kufanya
maana yake najua democratization si kama kahawa, ‘instant coffee’ ambayo
una brew una kunywa saa hiyo hiyo, it’s a process it takes a long
time.”
0 comments:
Post a Comment