Na Joseph
Ongong’a
Mchungaji Benjamin Bukuku |
Jumapili iliyopita idadi ya huduma katika Jiji la Dar es
salaam imeongezeka ambapo kiongozi wa huduma ya kweli itakuweka huru Mchungaji
Benjamin Bukuku yenye makao makuu yake mjini moshi hatimaye ameingia jijini Dar
es salaam ambapo ameanzisha kazi mpya lengo likiwa ni kuwaleta watu wengi kwa
bwana Yesu.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliweza kufurika
katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ulioko maeneo ya Bamaga Mwenge ambapo
katika hali isiyokuwa ya kawaida Kanisa hilo limeanza na kwaya kabisa jambo
linaloonyesha kuwa walijipanga muda mrefu kiasi kwamba kuna uwezekano mkubwa
kuwa huduma hii ikawa tishio kwa huduma zingine ambazo zimeanza siku nyingi
lakini ukuaji wake unakuwa wa kusua sua.
Huduma hiyo ambayo inajulikana kwa jina la kweli itakuweka
huru imejikita zaidi katika kuwafundisha watu kuijua kweli ya Neno la Mungu
ambapo watu wakishaijua matatizo yao mbalimbali yanaondoka hata bila kuombewa
ambapo jumapili iliyopita nyakati ilichuhudia jinsi mamia ya watu walivyokuwa
wakifunguliwa mara baada ya mafundisho hali ambayo inahatarisha baadhi ya
huduma ambazo zimekuwa zikitumia mfumo wa vitu katika kuwafungua watu.
Mchungaji Benjamin Bukuku akifafanua jambo |
Akiongea na Nyakati mara baada ya Ibada
kumalizika Mchungaji Bukuku alisema ameamua kuja Dar es salaam ili kuudhirishia
ulimwengu kuwa Yesu anaweza lengo likiwa ni kuwafumbua watu macho watoke gizani
kwani kazi ambayo naanza nayo ni kuwafundisha watu kweli na kuachana na
sarakasi zingine kwani watu wakishaifahamu kweli hakika matatizo kama ya
Magonjwa na mengineyo yanaondoka yenyewe na hii ndio iliyonisaidia hata mimi
mara baada ya kuifahamu kweli niliwekwa huru kabisa hivyo ninayofundisha ndiyo
ninayoyaishi hivyo wakazi wa Dar es salaam nawaomba waniunge mkono katika ibada
zetu zinazofanyika katika ukumbi wa chuo cha ustawi wa jamii ulioko bamaga
mwenge kila jumapilia kuanzia saa moja hadi saa tatu asubuhi
0 comments:
Post a Comment