PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Matokeo ya kidato cha nne 2012 kusahihishwa upya: Taarifa ya Serikali


  • Waziri atoa neema kwa wanafunzi waliofeli.
  • Pigo  ni kwa wale wanafunzi waliojinyonga


Na Joseph Ongong’a


Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Taarifa ya Tume ya uchunguzi wa matokeo cha nne 2012, iliyotolewa bungeni leo na Waziri wa nchi Ofisi ya waziri Mkuu, Wilium Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu, imesema kuwa tume imebaini kuwa mfumo mpya wa ukokotoaji uliotumika mwaka huu, wa kuongeza  alama za ufaulu tofauti na ule uliotumika miaka ya nyuma uliozingatia continue assessment, haukuwapa fursa ya maandalizi, kwa wadau, na haukufanyiwa uchunguzi yakinifu, kwahiyo tume hiyo imependekeza matokeo hayo yafutwe na kuangaliwa upya ili wanafunzi waliokosa nafasi wapate nafasi. Hivyo tume imefuta matokeo na sasa yanasahihishwa upya.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: