Mili ya watu 17 imepatikana hadi sasa. Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Meck Sadick, amesema kuwa kati ya miili hiyo wapo watoto wawili wa
Kiasia waliokuwa wakicheza katika eneo hilo, kati ya wanne wanaoendeleatafutwa.
Majeruhi waliookolewa ni 18, kati yao 10 wamelazwa katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili. Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema
hawategemei tena kupata watu wengine waliohai katika kifusi hicho. Wajenzi wa jamhuri wa watu wa China ndio walioonekana kuleta matumaini ya uokoaji, hata hivyo bado kuna maswali mengi kuwa kwanini serikali haikuweza kuwatafuta mapema? Ili uokaji kwa watu walio hai ufanikiwe? J&M Wamoja itaendelea kukuletea matukio mengi zaidi. Endelea kufuatilia.
0 comments:
Post a Comment