Bwana ndiye Mchungaji wangu
sintapungukiwa na kitu…..uhisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia ya
haki kwa ajili ya jina lake …… Zab. 23….
Huu ni sehemu ya wimbo wa mtu mmoja jasiri aliyejibeba sifa kemkemu kutokana na
ujasiri na ushupavu wake katika vita. Nami mchambuzi wako jasiri Joseph
Ongong’a, ningependa nitumie beti chache za wimbo huo, hasa ninapoendelea
kuandika makala hizi zinazohusu mashujaa wa imnai wa wakati huu, ambao
wanaoteswa kwa ajili ya imani yao…..
Kabla ya kusonga mbele na hoja yangu,
ningependa niwashukuru wasomaji wangu ambao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu makala haya. Wiki iliyopita nilipokea jumbe
kadha wa kadha kupitia simu yangu ya mkononi huku wengine wakadiriki kunipigia simu kwa kunipongeza kwa
ujasiri wangu wa kueleza ukweli kuhusu wanaoteswa kwa ajili ya imani yao. Na
baadhi walichangia mawazo yao wakinitaka nifanye marekebisho kidogo
yaliyotokana na makosa ya kiufundi katika makala ya “BOKO HARAMU Tanuru
linalomeza Wakristo Nigeria.” Napenda kukubaliana nao na kusahihisha kuwa,
Wakristo walioko katika nchi hiyo wako upande wa Kusini na siyo Kaskazini kama
ilivyosomeka.
Mwana Fizikia mmoja alitoa kanuni
yake ya mwendo akisema: “Katika kila tendo kuna usawa na mkwaruzo au ukinzani,
ule unaopingana na usawa. Alikwenda mbele zaidi kwakusema kuwa, “laiti kama
kusingekuwepo na misuguano duniani watu
wasingeweza kutembea juu ya uso wa dunia,” kungetokea utelezi ambao usingekuwa
na ukomo wake. Huu usemi unadhihirisha wazi kuwa, migongano inaweza kuwa ni sehemu ya maendeleo.
Katika safari ya makala haya kuna
baadhi waliojitokeza na kuniandikia ujumbe mfupi wa Maneno wakieleza kukereheka
na makala haya yanayohusu mateso ya wafia imani(wakristo), wakinitaka niachane
nayo mara moja, huku wengine wakinitishia maisha, mimi sintaogopa mabaya yote. Mfano
mwenye simu namba 0655131955; aliandika ujumbe mrefu akisema; “Bwana Joseph, tatizo kubwa linaloikumba
jamii yetu hasa wakristo, ni kutokuwa wakweli, huu mtindo wa kuandika habari za
propaganda na uongo ndio zimefikisha mataifa mengi katika mauaji ya kutisha.
Angalia madhalimu wa kiisraeli wanavyoua watu ovyo na watu wa aina yako
hukaa kimya na muda mwingine
kupongeza mauaji hayo, na hii ndio inayotukia hata hapa tz. Mmejazwa
propaganda tu,” alisema na kuendelea: Marafiki zenu wa Kimarekani wameua
mamilioni wangapi wa Kiislamu Iraq, Afghanistan, Pakistan, Somalia na
kwingineko? Ujue amani haimbwi amani inatokana na haki kama kuna watu
mnawadhulumu siku zote ipo siku wata kata tama na hapo huwa ni chanzo cha
uvunjifu wa amani. Tz wanadhulumiwa
waislamu kwenye elimu, mamlaka na mikataba ya upendeleo baina ya
serikali na makanisa haya hamyazungumzi, hamuoni kama sehemu ya dhuluma, siku
watu wakikata tamaa ni tatizo. Kataeni upendeleo huo na amani itakuja yenyewe.
Mwengine aliyeandika ni mwenye
namba za simu: 0777842132; yeye naye
alisema: Ww una chz 2. Wachana na BOKO HARAMU bwege nn?. Hizo ndizo ujumbe
nilizopokea kati ya nyingi nilizotumiwa, unaweza ukapata picha kamili kwa sasa
kile nilichoanza kukizungumzia tangu kuanza kwa makala hizi.
Damu na uhai wa wakristo eti
unaangamizwa kwasababu ya hayo waliyojaribiwa kuyaelezwa hapo juu, mimi sioni
kama kuna sababu ya msingi hapo hata kidogo. Mfano mzuri hebu soma habari ya
mwanamke huyu, ambaye amepata majeraha ya kutisha kwenye mikono na viganja
vyake baada ya kuunguzwa na mumewe kwakosa tu la kujiunga na ukristo. Je hapo
kuna suala la elimu. Fikiria kwamba pamoja na mateso mwanamke huyo ameendelea
kunga’ng’nia imani yake hiyo, huku akijitia moyo na maandiko yasemayo: Ni kitu
gani kitatutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au njaa, au mateso au
mavazi…… anasena hakuna hata kidogo! Rumi 8:35.
Ukweli ni kwamba Wakristo
wanateswa, huku wakiendelea kutiwa moyo tu na maandiko kutoka katika kile
wanachoamini kuwa, maisha yao siyo ya hapa duniani, kwani wao wanayachukulia
mateso ya sasa kama kitu kinachotokea punde tu na kuwa wanayo matarajio makubwa
zaidi na faraja watakayopata baada ya maisha haya ya mwili. “Wanaolia sasa
watafutwa machozi yao, na wale wanaofurahi sasa na kutesa wenzao, kwa ajili ya
haki, watalia na kusaga meno hapo baadaye.” Wiki ijayo nitakuletea makala inayomhusu
mwanamke huyo kwa kina zaidi.
0 comments:
Post a Comment