Tanuru linalomeza
Wakristo Nigeria!
Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA
humponya nayo yote, Huifadhi mifupa yake yote (Zab.34:19),” Maneno haya kutoka
katika Biblia takatifu, yanafaa sana kumtia moyo yule anayepitia kwenye
majaribu kama daraja la kuvukia. Mara nyingi mistari hii imetumika katika
kuonesha hisia au huzuni kwa yule anayekutana na adha fulani, hasa mwenye haki. Kwa Maneno hayo, nikualike sasa kwenye makala haya ili uungane
nami Joseph Ongong’a kuwatia moyo na kuwaombea Wanaijeria wenzetu, walioko
kwenye mateso makali ndani ya tanuru la BOKO HARAM…
Mateso
ya kidini katika maeneo mengi ulimwenguni ni matukio ya kawaida sana katika historia ya binadamu. Kutukanwa,
kudharauliwa au kuuawa kwa sababu ya kutofautiana kiimani, kukorofishana,
kugishana au sababu yoyote ile, ni jambo
la kwaida sana kwa jamii ya Wakristo hivi leo. Wakati kikundi cha fulani cha kidini kinapoamua kukiangamiza
kingine kikidhani kuwa kufanya hivyo ni kutetea imani yake.
Wakati wa mateso haya ya kiimani yanapotokea mambo mengi
huwa hujitokeza , isipokuwa tu katika nchi ambayo Serikali yake inamtazamo
mzuri katika kuijali raia wake. Mara nyingi katika baadhi ya nchi makundi hatari dhidi ya zingine zimeibuka ambayo yamekuwa yakidai kuwa kwakutesa,
kuchinja na kuteketeza kwa moto wenzao wa imani nyingine wanatekeleza amri ya
mwenyezi Mungu.
Watu wa Mungu walioishi kipindi cha Agano la
kale, Ibrahim, Nabii Musa na watumishi wengine, wakati Yesu Kristo na
hata walioishi katika kipindi cha matendo ya mitume, waliopitia kwenye mateso mengi ya imani
kulingana na wakati wao. Dunia, ardhi ileile walilolikalia baddo ipo, watu wema na waovu bado wapo, Wanaopenda na wasiopenda sheria ya Mungu
wapo, hivyo mateso ya kiimani ni dhahiri na
yanaendelea kamakawaida.
Zaidi ya miaka 10 kuanzia miaka ya 1990, Wanaigeria zaidi ya 12,000,
wamepoteza maisha yao kutokana na vita vya kidini kati ya Wakristo na Waislamu.
Nigeria ni nchi ambayo iko katika mikondo miwili, eneo la kusini ambalo
linakaliwa na Waiuslamu na eneo la Kaskazini wanapokaa wale wa imani ya
Kikristo. Kinachosikitika hapa ni pale
mateso makali yanaelekezwa upande wa Kaskazini wanapoisha Wakristo.
Waumini wanalazimishwa na serikali kukutana katika vikundi vidogovidogo, ili kuepuka
mashambulizi yanyoweza kufanywa dhidi yao . Wakati mwingine wamekuwa wakipigwa
na kufungwa gerezani na wengine kufia huko.
Wakristo walioko Nigeria wanapita
katika tanuru kali la moto kutoka kwa kundi hatari la BOKO HARAM, ambalo
linakusudia kuifuta ukrtisto nchini humo. Kundi hilo ambalo linasadikika kuwa
ni la Kiislamu lenye imani, limekuwa likifanya mauaji ya kutisha, kwa
jamii ya Wakristio ikiwa ni pamoja na kuchoma majengo ya ibada kwakuyalipia
mabomu.
Katika kutekeleza hazma yao ya kutaka kufuta ukristo nchini
Nigeria, kundi hilo liliwateketeza kwa moto zaidi ya Wakriso 50, mbele ya
Mchungaji, wao katika nyumba yake walipokutanika wakijificha na kufanya maombi
kwa hofu ya kukamatwa. Katika shambulio hilo, lilimkumnba mama Mchungaji aliyeteketea vibaya na mtoto
wake akiwa pembeni mwake. Baada ya shambulio hilo, Mchungaji wa kanisa hilo la
Kipentekoste Rev. Dachollom Datiri,
alinukuliwa
akilalamikia serikali ya nchi hiyo
kushindwa kudhibiti hali hiyo na kuwaacha Waislamu kuwashambulia
Wakristo kila Jumapili, tena wakati wanapofanya Ibada ya kumtukuza Mungu wao.
“Tunaonewa sana, ibada zetu hazithaminiwi hata kidogo,
tunashambuliwa, tena tukiwa ibadani, tuanuawa kila kukicha, na tumejaribu
kujitenga lakini bado tunafwatwa na kuchokozwa, wakati sisi tukiwa kimya na wa
pole,” alilalamika Mchungaji huyo.
Nigeria ni nchi iliyoko Afrika na taarifa kutoka mtandao wa
haki za binadamu Marekani zinaeleza kuwa, nchi hiyo imekuwa ni taifa hatari kwa
mauaji ya wakristo. Inasemekana mamia ya Wakristo wakiwemo wanawake na watoto wametekwa na
kundi la Boko Haram. Hata hivyo kundi hilo limenukuliwa likisema: Tunawataka
Wakristo wote mgeuke na kuwa Waislamu la! Hamtakuwa na amani kamwe katika
maisha yenu (All Christians need to turn to Islam or 'they would never know
peace again).' kilisema na kuongeza; Mpango wetu na mkakati wetu ni kuifanya
nchi ya Nigeria kuongozwa na Shariah, na siyo vinginevyo.”
“Tuta hakikisha kwamba, tunawafukuza Wakristo wote waishio
Kaskazini na kutangaza utawala wa Shariah ya kiislamu nchini Nigeria,” kilisema
kikundi hicho.
0 comments:
Post a Comment