TB Joshua, ambaye ujumbe wake unatarajiwa kuja nchini kesho Mwandishi Wetu
WAINJILISTI sita kutoka kwa Nabii maarufu duniani, TB Joshua wa Kanisa la The Synagogue Church of all Nations ( Scoan) la nchini Nigeria wanawasili nchini kesho Jumapili kwa ajili ya shughuli za injili.
Wainjilisti hao wanakuja nchini kwa ajili ya shughuli maalum za injili ambapo wataonana na waumini mbalimbali wa Kanisa hilo waliopo hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Kanisa hilo hapa nchini, Martha Kaaya, alisema Kanisa hilo lina makao yake makuu mjini Lagos, Nigeria.
Martha alisema wainjilisti hao ambao watawasili kesho watakaa kwa siku nne wakifanya kazi ya kuwasaili watu wanaotaka kwenda nchini Nigeria kwa maombezi.
Alisema kuna watanzania wapatao 400 ambao wameomba kwenda kupata huduma ya maombezi kwa Nabii TB Joshua kwa ajili ya maombezi na matatizo kiroho na kimwili.
“Wainjilisti wataonana na watu waliojiandikisha kwenda Scoan Nigeria kwa maombezi tarehe 27, waje na ripoti za kitabibu na wawahi asubuhi sana ili kuwahi usaili,” alisema Martha.
Alisema siku ya Jumanne Agosti 28 na Jumatano Agosti 29 wainjilisti hao wataonana pia na marafiki na wadau wa televisheni ya EMMANUEL saa 2.00 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubelee na aliwaomba watu wote wawaahi kufika ukumbini kabla ya saa mbili asubuhi.
Alisema kati ya watu 400 walioomba kwenda kwa Nabii TB Joshua, watakaoshinda kwenye usaili huo ndio watakaoenda nchini Nigeria kwa mwaliko wa nabii huyo. |
|
Chanzo cha habari hizi ni kwa msaada wa mtandao wa mtandao wa Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment