Everton wamejiweka katika nafasi nzuri hatua ya makundi kufuzu kwa kombe la ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Wamewabamiza Hajduk Split bao mbili kwa bila ijapokuwa mechi
ililazimika kusimama kwa dakika kadhaa kutokana na vurugu za mashabiki. Katika
dakika ya 33 ya mchezo, mashabiki wa Hajduk walisogea uwanjani na kurusha vitu.
Meneja wa Everton Ronald Koeman amesema amesikitishwa na tukio
hilo ingawa hakujua ni nini kimetokea.
Dakika tatu kabla ya vurugu kutokea Michael Keane alikuwa
amewachapa bao la kwanza, na mara baada ya kutuliza vurugu zao Idrissa Gueye
akawachapa la pili dakika ya 45.
Katika mechi nyingine, Ajax wamekutana na changamoto baada ya
kubamizwa goli moja bila na Rosenborg kutoka Norway.
Mwezi May Ajax walipigwa na Manchester United kisha wakampoteza
meneja wao Peter Bosz aliyetimkia Borussia Dortmund na pia Captain wao Klaassen
akenda zake Everton.
0 comments:
Post a Comment