PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Watu 108 Amani Christian Centre wakaribisha 2014 na utu mpya!



·    Ni baada ya kuuzika utu wa zamani
·    Askofu asema ni zawadi ya mwaka 2014
JUMAPILI ya Desemba 22, mwaka huu, katika kanisa la Tanzania Assemblies of God, Amani Christian Centre, Tabata jijini Dar es Salaam,  vifijo nderemo na shangwe vilitawala, wakati ambapo watu 108, waliokoka katika semina iliyofanyika kaniania hapo  walipoamaua kubatizwa kwa maji mengi, kama tendo la kuuzika utu wa kale na kuuvaa utu mpya. Ungna na Mwandishi wa makala hii, Joseph Herman, ili akujuze zaidi.

Askofu Dk. Lawrence Kametta, akiwaongoza sala ya toba baadhi ya watu waliookoka katika ibada ya Jumapili kanisani hapo wiki iliyopita
Awali kabla ya kuingia katika zoezi hilo la kubatizwa kwa watu hao, Mchungaji na Mmisionari, Adama Haji, kutoka Somalia, alifundisha waumini hao, somo lililohusu, “kutambua vipawa na jinsi ya kuvitumia katika kuleta mabadiliko ya maisha,” na kuwataka waumini hao wanazitumia vizuri zawadi hizo walizopewa na Mungu kwa maslahi ya kanisa na taifa kwa ujumla.
Mtumishi huyo wa Mungu alisema kuwa, Mungu hakumuumba  mtu ili aishi kwa hasara na baadaye kutoweka hapa duniani akiwa na nguvu, kipawa  akiwa hajaacha  historia yoyote,  bali  alete mabadiliko itakayofaidisha wengi.
 “Kanisa la leo liko katika hali mbaya kiuchumi na hata kiroho, kwa vile yupo mtu mmoja ambaye ameamua kuzika kipawa chake na hayuko tayari  kuachilia ifanye kazi na kuleta mabadiliko,” alisema Haji.
Aidha alisema, funguo za mabadiliko ya maisha ya kila mtu, ziko katika maarifa, ambayo yanapatika kwenye Neno la Mungu kama kitabu cha Hosea 4:6 inavyo fafanua, na katika elimu nyingine ya kawaida, ambapo  aliwasisitizia  waumini hao kuendelea kutafuta edlimu bila kujali umri wao.
Ask. Dk. Kametta na Mchungaji Adam Haji wakibatiza
“Nasema siku utakapoacha kusoma, ndipo utaacha kuishi, ni aibu kwa mtu mwenye umria wa miaka 35 anaacha kusoma, tujiadhari sana na dunia hii ya sasa kwani bila kutafuta maarifa tutashindwa kukabiliana nayo, na hata sisi watumishi wa Mungu, tusipotafuta maarifa, tutashindwa kuwaongoza waumi wetu,” alisema Haji, na  kuongeza: “Tumia kipawa chako ipasavyo, kama ni kusoma soma kwabidii, na kama una kipawa cha kuchekesha na kucheza mpira cheza kwa bidii usikubali kukizika.”

Jengo la Kisasa la Kanisa la TAG Amani CC, Tabata
Naye  Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini, Dk. Lawrence Kameta, akifundisha kuhusu ubatizo, wa maji mengi alisema kuwa, hakuna njia nyingine mbadala ya ubatizo ambayo wakristo wanapaswa kufuata isipokuwa ni ile aliobatiziwa Yesu Kristo.
Askofu huyo alisema kuwa, kuna baadhi ya watu wamepotoshwa na injili zingine  ambazo zinakazia juu ya mafanikio na siyo neno sahihi, linalowaongoza  kwenye kuishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu, yanayomfikisha mtu mbinguni.
Watumishi wa Mungu wakishukuru baada ya ibada ya ubatizo
Aliwataka waumini hao kukubali na kutii neno la Mungu, linalowaelekeza kwenye kweli ya Mungu, na kuepuka mafundisho yasiyofaa, zinazolaghai na kuwatenga mbali na uso wa BWANA.
Kanisa hilo ambalo kwa sasa linaabudia katika jengo la muda kupisha ujenzi wa Jengo kubwa la kisasa unaoendelea, wana ibada tatu, ambayo ibada ya kwanza ni ya Kiingereza, inaanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 2:00, na ya pili ni kiingereza inayotafsiriwa kwa Kiswahili  inaanza Saa 2:00 hadi saa 9:00 na ibada ya tatu ni ya Kiswahili, yenyewe inaanza saa 9:00 hadi Saa 6:00 mchana.
Wasiliana nao kwa simu No: 0784374026

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: