PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Binti wa miaka 16 ajinyonga Dar.

Na Joseph Herman
 
Binti wa miaka 16 aliyejulikana kwa jina la Zayana Mwamini amekutwa amejinyonga juu ya mti ulioko jirani na Rondo Gesti, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

 Kwa tarifa ambazo zimeifikia mtandao huu kutoka kwa dada wa binti huyo,  Shamu Burohani,  alisema kuwa, Zayana, alikutwa asubuhi Desemba 18 Mwaka huu akiwa amejinyonga na kamba za manila juu ya mti huo na mwili wake ulichukuliwa na Askari Polisi wa Kizuiani(maturubai) kwa uchunguzi zaidi.

 Shamu alisema sababu ya mdogo wake kujinyonga ilitokana na kugombezwa kutokana na tabia yake ya kutoka hapo nyumbani, bila kuaga, ndipo alipopata hasira na kuondoka hapo nyumbani Desemba 17 mwaka huu saa 5 asubuhi.

.“Baada ya kuondoka tulipoona harudi tulichukua hatua ya kumtafuta, bila mafanikio, ndipo ilipofika asubuhi ya Desemba 18, mwaka huu, majirani walituambia kuwa wamemuona juu ya mti ulioko na jirani na gesti ya Rondo, akiwa amejinyonga na kamba ya manila,” alisema Sham.
Shamu alisema kuwa ameishi na mdogo wake kwa miezi miwili sasa na kuwa alikuwa najifunza ufundi wa kushona nguo, lakini  alianza tabia ya kutoka na kulala nje bila sababu yoyote .

Mwili wa binti huyo ulichukuliwa na Askari Polisi wa kituo cha Mbagala Kizuiani(maturubai) kwa uchunguzi zaidi.


Baadhi ya Mashuhuda wakiangalia mwili wa Zayana, aliyejinyonga kwa kamba.


Askari Polisi wakipakia Mwili wa Zayana  katika gari.


Askari Polisi wakishusha mwili wa Zayana kutoka katika mti(Picha zote na Mathias Charles)

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: