Watu wanaosadikika kuwa ni magaidi wamevamia Jengo la kibiashara la Westgate lililoko Nairobi Kenya na kuua watu zaidi ya 30 na wengine zaidia ya 70 kujeruhiwa. Habari zilizoifikia mtandao huu mpaka sasa zilieleza kwamba watu hao wanaosadikiwa kuwa walikuwa kama 10 hivi walivamia jengo hilo la kibiashara majira ya saa 6.20 mchana wakiwa na silaha kali za kijeshi na kuanza mashambulizi kwa watu mbalimbali wanaofanya shughuli zao ndani ya Jengo hilo. Hata hivyo haijafahamika vizuri ni kwanini wavamizi hao walikivamia jengo hilo na walikuwa na sababu zipi za msingi.
Baadhi ya manusura wamesema kuwa watu hao walikuwa wanaongea lugha ambayo siyo ya kiswahili wala kiingereza bali waliongea lugha yao isiyofahamika.
Jengo la WESTGATE |
Wengine walidai kuwa walikuwa ni watu wenye asili ya kiarabu na walisikika wakiwaanmbia watu waliokuwemo ndani ya jengo hilo kuwa wanawatafuta wale wasio Waislamu. Wakidai kuwa ikiwa wewe ni Muislamu wasinge patikana na madhara lakini kinyume na hapo wanashambuliwa.Polisi na Jeshi la Kenya bada wanahaha kuwasaka watu hao bila mafanikio
0 comments:
Post a Comment