PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Askofu Dk. Kulola Afariki Dunia, Aagwa na Maelfu ya watu Dar.

  • Viongozi mbalimbali wa  serikali, dini na siasa wampongeza
  • Wengi wasema walimwamini Mungu kupitia mikutani yake
  • Dk.Ally Mohamed Balal akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Dk. Kulola
  • Askofu Zakaria Kakobe atoa ya moyoni, awataka watu  kuwa wazi
Msiba wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God,  umewavuta watu wengi, viongozi wa serikali na siasa kutoka kila pande nchini Tanzania. Wengi wametoa salamu zao za rambirambi wakionesha jinsi ambavyo Askofu Kulola alivyokuwa mtu wa watu na mpenda amani.

 Akiongea wakati wa kutoa heshima za mwisho za kumwaaga mkuu huyo wa dini, Temeke jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Alli Mohamed Balal, alisema kuwa, Askofu kulola alikuwa ni mtu wa watu aliyehubiri inili ya kweli, iliyoleta mstakabali wa amani ya nchi hii.
Makamu huyo wa rais aliwataka waumini wote wa waliosalia kumuenzi askofu Kulola.
Mjane wa Dk. Kulola akifarijiwa na mmoja wa viongozi wa Sertikali

Viongozi mbalimbali wa dini, na sisa waliohudhuria msiba huo walitoa salaamu zao za rambirambi, huku Askofu Zachary Kakobe akitoa ya moyoni aliposema kuwa, njia iliyo sahihi kwa watu wote ni kumwamini BWANA Yesu, na kuwataka wote wakiwemo viongozi wa sisa na serikali waliohudhuria na kutoa salaamu zao kumkiri Yesu hadharani pasipo kujificha na kujitokeza siku ya msiba.

Kakobe alisema kuwa, Dk.Kulola amemaliza kazi yake, kazi imesalia kwa walioko hai ambao wanatakiwa kumwamini Yesu na kujitoa kwa haki pasipo unafiki. 

Mwili wa Dk. Moses Kulola, utasafirishwa kesho kuelekea Mwanza kwa mazishi yakayofanyika siku ya Jumatano katika eneo la kanisa la  Capri point jijini . 

Askofu Kulola, alifariki siku ya Alhamisi katika kituo cha afya cha AMI, kilichoko Masaki jijini Dar es Salaam, kwa ugonjwa wa ini na figo.  

 
  
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: