Misri ni taifa lenye historia kubwa kwa
wakristo, kabla ya Kristo ( KK), na baada ya (BK). Biblia kwa sehemu ya
Agano la kale, taifa hili limeizungumziwa kama mahala pa uhamisho, kwa wana wa
Israel, walipoishi wakiteswa vikali, agano jipya nalo linaitaja kama mahali pa
maficho ya Kristo Yesu, wakati mfalume Herode, alipotaka uhai wake. Ungana nami
mchambuzi wako Joseph Ongong’a, ujue hali ilivyo kwa Wakristo huko Misri….
“Nilikuwa nahubiri habari njema ya wokovu na toba, kwa
lengo la kuleta uponyaji kwa taifa hili, nikidhani kuwa zinapendwa na wengi
na ndizo habari pekee, zinazoweza kugeuza mioyo ya watu na kubadilisha
mienendo mibovu ya maisha yao, lakini
nimeishia mikononi mwa polisi, kufikishwa mahakamani na baadae kufungwa
jela,” ndivyo alivyonukuliwa Bw. Abdel Kamel, 61, mkristo raia wa Misri aliyewekwa kizuizini kwa kosa la
kugawa vipeperushi vyenye kutangaza injli.
Kamel ambaye ni Mkristo, alikamatwa na polisi katika mji
wa Cairo, akiwa na kopi za vipeperushi zenye kueneza Injili na kuhukumiwa
kwenda jela kwa siku nne kwa madai ya kuvunja sheria ya nchi kwa kugawa
machapisho yenye maandiko ya kidini kwenye eneo la wazi barabarani.
Hata hivyo alipofikishwa polisi alilalamika kuonewa
akisema, Waislamu wao wanakawaida ya kugawa machapisho yao bila kusumbuliwa
na mtu yeyote, lakini askari hao walimpuuza na kumwambia kuwa, ni sawa lakini
kwa wakristo ni kosa.
Kamel aliachiliwa
huru siku nne daadae baada ya Mahakama kuona hana na hatia, hata hivyo
walikusudia kumsumbua kwa sababu ya chuki za kiimani dhidi ya wakristo.
Alisema kuwa Polisi hao waliomkuta akifanya huduma hiyo ya Mungu, pembezoni
mwa barabara, wakamchukua na kutupa katika haradinga lao wakampiga na
kumkimbiza katika kituo cha polisi.
Kwa upande wake Mwanasheria Nabil
Ghobreyal, aliyeshugulikia kesi hiyo hadi Kamel, alipoachiwa huru, alisema
kuwa, katika nchi ya Misri, hakuna sheria kama hiyo inayo kataza usambazaji
wa vifaa vya kidini au injli.
Baadhi ya watu na wakristo
waliochukizwa na jambo hilo, walisikika wakisema kuwa, kuhubiri Neno la Mungu
linalotangaza msamaha wa Kristo, kwa wenye dhambi, unatendwa vibaya kama mtu
aliyekutwa vitu haramu. “Tunasikitishwa sana na matukio kama haya, kwani
Wakrito toka enzi za mababu zetu tunasikia wanaishi huku wakichukiwa na
wengi,” alisema Kamel na kuongeza,
huku akisisitiza akisema:” I love my
people, I love Egypt, and I feel my service is directed towards the people I
love and the country I love,” akimaanisha kuwa, Nawapenda watu wangu,
naipenda Misri na nahisi huduma yangu kuelekezwa kwa watu ninaowapenda na
nchi ninayoipenda sana.
“Mamlaka
ya nchi ilimtia Kamel kwa siku tatu
bila kumwachia na hata kumnyima haki ya kuonana na familia nyake na
mwanasheria wake. Na siyo tu hivyo ilimkataza hata kupata chakula, dawa kwa
ajili ya afya yake kwa muda huo wote, haikumtendea haki, kwani mtumishi huyo
ni mtu mstaarabu na mpenda Mungu na hana tuhuma zozote zile,” alisema
mwanasheria wake.
Baadhi ya watu wengine wanaopenda ukristo walisema kuwa wakati Kamel alipowekwa kizuizini, polisi walifika kwake kila wakati usiku wakidai kufanya upelelezi na upekuzi, wakichunguza machapissho yote kana kwamba alikuwa amefanya jambo zito la kushtua sana. Tunachokishangaa hapa ni pale tunapoona Injili ambayo inabeba ujumbe wa amani, ambayo haina hila yoyote, inasumbuliwa kiasi hicho, kitu ambacho sicho kizuri kabisa. Alisema kuwa kuna uonevu makubwa sana kwa Wakristo nchini Misri kwenye upande wa uhuru wa dini, kwani kwa Waislamu wanaruhusiwa kueneza dini yao wakitumia vitabu, majarida na hata kwa kutumia vipaza sauti vilivyotundikwa nje ya Misikiti yao, na wanapofanya hivyo hawaulizwi na mtu yoyote bali inapotokea kwa upande wa Wakristo inakuwa ni taitzo kubwa, wanakatazwa hata kushirikiana kwa masuala ya imani yao inasikitisha kuona binadamu waliumbwa na Mungu, na anakiri kumtumikia kumbagua mwenziye kiasi hicho.
“Why, when we are doing it, are we
not even allowed to put our view across?” he said. “Why aren’t we treated the
same?” alisisitiza.
Aidha Kamel anashukuru juhudi za vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya jamii vilivyochapisha tukio hilo na kutia msukumo mpaka akaachiliwa huru. Nadhani waliamua kuniachilia huru kwa vile waliogopa baada ya kuona vyombo vinaripoti tukio hilo kwa kasi kubwa duniani kote.
Kwakweli mateso yanayowapata
Wakristo waishio Misri ni mwendelezo wa chuki dhidi yao, tangu miaka mingi
iliyopita, enzi za utawala wa Farao mababu wa imani wa kikristo hali
haijatulia hadi sasa, kwa kunawakati wanatubagua na kutuita kuwa sisi ni wakimbizi
tu tuliosalia, haijalishi hata kama umezaliwa na mmisri mwenzio,” alisema
Kamel.
Nchi yetu ya Misri wakati wa
utawala wa Rais Husen Mbarak, matukio ya kiubaguzi hayakuwepo kwa kiwango cha
juu, kama tunavyoanza kuona wakati huu ambapo rais mpya Mohamed Morsi's, kuutangazia umma
kuwa, yeye atakuwa Farao mpya wa Misri,” alisema Kumel na kuongeza: Tumeanza
kuonja makucha yake kwani ameamua kubadili hata katiba ya nchi ambayo
tunaamini kuwa itatetea maslahi ya waislamu ikiwa chini ya sharia.
Huyu anaweza akawa kama Farao
asiye mjua Yusufu, ambaye kamwe hata
kubali kuachia watu wa Mungu waweze kumwabudu Mungu, wao kwa uhuru,na kwa
amani inawezekana akachukua hata vitabu vya kumbukumbu kuchunguza pale
walipoacha na kusahau kufuata desturi yao kama ilivyokuwa awali, tunawaomba
wakristo wenzetu ambao bado wanaouhuru wa kuabudu kutukumbuka katika maombi.
wakristo na Waislamu waliishi kwa amani na upendo na matukio ya
kubaguliwa hayakuwepo katika
|
Alisema hayo baada ya mahakama ya nchi hyo kuihukumu familia
ya watu 15, kwenda jela kwa kosa la kuahama uislamu na kujiunga na ukristo
0 comments:
Post a Comment