- Ø Sasa yuko huru na familia yake
- Ø Mataifa mengi yasherehekea ushindi huo
- Ø Yasema Mungu ametenda makuu
Na Joseph H. Ongong’a na Mashirika ya habari
MAHAKAMA ya Iran imemwachia huru Mchungaji raia wa Iran, Youcef Nadarkhani, aliyekabiliwa na hukumu ya kifo kwa kosa la kusaliti dini ya Kiislamu baada ya kubaini kuwa hana kosa isipokuwa imemhukumu jela miaka mitatu, ambayo tayari aliisha itumikia.
Mchungaji Youcef Nadarkhan |
Mahakama hiyo ilimwachia huru Mchungaji Youcef, Jumamosi, baada ya kukaa gerezani kwa takribani miaka mitatu, na sasa Mchungaji huyo amerejea nyumbani kwake kuungana na familia yake huko nyumbani kwake Rasht.
Wakili wa Mchungaji huyo alieleza kwamba, pamoja kuachiwa huru, lakini pia mahakama hiyo ilimhukumu Youcef Nadarkhan, kwenda jela miaka mitatu, baada ya kupatikana na hatia ya kumhubiri Muislamu na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu ambapo hata hivyo aliachiwa huru kutoakana na kwamba kifungo hicho alikuwa amekwisha kitumikia.
Mchungaji Nadarkhani, (33), ambaye ni Muislamu kwa kuzaliwa alikamatwa Mwaka 2009 akiwa mjini kwake huko Rasht kusini mwa Iran, wakati akiwa na kanisa lake la watu 400. Inasadikika kuwa alibadili dini na kuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 19.
Mchungaji Youcef Nadarkan akilakiwa na familia yake mara baada ya kuachiwa huru |
Aidha alihukumiwa kifo Mwaka 2010, na mwaka 2011, Mahakama Kuu ya Iran ilimtaka Nadarkhan kuikana dini ya ukristo na kurejea Uislamu, jambo ambalo halikuwezekana kabisa hadi alipoachiliwa huru.
0 comments:
Post a Comment