Na Samwel Thomas
MOJA ya changamoto kubwa inayo
likabiri taifa la Tanzania katika sekta mbalimbali hapa nchini ni kukidhiri kwa
rushwa, hivyo wataalamu wa ubunifu wa majengo na wakadiriaji majenzi nchini
wametakiwa kuepuka changamoto hiyo ili waweze kufanya kazi yao kwa weledi na
uadilifu ili wapate fursa ya kudhaminiwa katika jamii ya Tanzania.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert E. Mringo wakati akifungua semina ya waataalamu
hao waliokutana jijini Dar es Salaam, kutoka mikoa yote ya Tanzania kwa lengo
la kujengewa uwezo katika ufanyaji wao wa kazi.
Balozi huyo ameongeza kuwa ili mtu
aweze kuheshimika na kuonekana mwenye maendeleeo katika shughuli anazo zifanya
ni lazima kuwa na heshima na katika kazi yake na kuepuka kuomba wala kutoa
rushwa kwa aina yoyote.
Ameongeza kuwa kumekuwa na baadhi
ya wafaanyakazi hapa nchini kushindwa kuzittumia nafasi walizopo katika kazi
zao na kujikuta wakiachishwa kazi kutokana kutokuwa na uadilifu ikiwa ni pamoja
na uendekeza masuala ya Rushwa hali inayo lisababishia taifa hasara kubwa na
kuzidi kudumaa kimaendeleo.
Sambamba na hilo amesema wataalamu
hao ni wa muhimu kwa kiwango kikubwa katika taifa la Tanzania lakini endapo
watashindwa kujitambua kazi yao itaonekana haina maana yoyote na kujikuta
wakipoteza kazi zao endapo hawata kuwa waaminifu na kupiga vita rushwa, ambayo
siku zote ni adui wa maendeleo.
Aidha baadhi ya washiriki wa semina
hiyo katika mahojiano maalumu wamesema kuwa semina hiyo itakuwa mchango mkubwa
kwao katika kuhakikisha kuwa wanajipanga kwa upya katika utendaji wao wa kazi,
huku wakiahidi kupambana na changamoto mbalimbali wanazo kumbana nazo.
Ubadhilifu uepukwe pembejeo za kilimo
Na Samwel Thomas
IMEELEZWA kuwa moja ya changamoto kubwa sekta ya kilimo
hapa nchini na kuifanya sekta hiyo izidi kudumaa zaidi ni kutokana na ubadilifu
mkubwa unaofanyika katika pembejeo za kilimo ikiwa ni pamoja wizi wa mbegu bora uhaba wa mbolea pamoja na
kuwepo kwa usimamizi mbovu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzzi
wa Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) Bi.Janeth Bitegeko wakati
akizungumza katika warsha ya wadau mbalimbali wa kilimo hapa nchini waliokutana
katika hotel ya Blue Pearl iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa ili
sekta ya kilimo hapa nchini iweze kuimarika na kuukua kwa lengo la kuleta
maendeleo kwa wakulima na kwa taifa kwa ujuumla ni lazima iwepo fursa ya
upatikanaji wa mbegu bora iwepo , mbolea pamoja na kuwepo kwa usimamizi wa kutosha
katika pembejeo za kilimo hapa nchini.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa
kilimo kitaalinufaisha taifa na kuondokana na tatizo la njaa pale tu Serikali
itakapo una umuhimu wa kuiangalia sekta hiyo muhimu hapa nchini kwa jicho pama
ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima katika maeneo mbalimbali ya tanzzania.
Amesema kuutokana na tafiti zilizo
fanyika zimebaini kuwa bado kilimo hakijapewa kipaumbele katika taifa hili
hivyo kuzidu kudumaa siku hadi siku, hivyo njia mbadala kuutakiwa kuchukuliwa
ili kukinusuru na kwaajili ya maaeendeleo ya mtanzania.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi na
Mwenyekiti wa sera na ushauri wa Baraza hilo la kilimo Tanzania Profesa Andrew
Temu amewataka wakulima kujikita zaidi
katika kilimo bora kwa lengo la kubadilisha hali yao ya uduni wa maisha.
Ifahamike kuwa nchi yoyote duniani
ili iweze kusonga mbele kimaendeleo lazima sekta ya kilimo izingatiwe, lakini
kwa taifa la Tanzania sekta hiyo imeonekana kuwekwa kando sikuhadi siku hivyo
taifa kuzidi kuwa masikini.
0 comments:
Post a Comment