BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo
Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi 3074 walioomba vyuo na mikopo
ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo kupitia
mitandao yao (website) Agosti 10 na
12, 2012 zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari mbalimbali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao imebaini kuwa na
mapungufu kadhaa katika maombi yao
ya kupewa mikopo ya vyuo.
Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo bodi imezibaini kwa
walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa
muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya
muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za
mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.
Kwa upande wake TCU imewaengua jumla ya waombaji 425 kwa
dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha katika taarifa yake.
Miongoni mwa dosari ambazo zimetajwa na TCU kwa wanafunzi
hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya
nne na tano (O' level na A' level Index number), miaka ya kumaliza masomo (year
of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji (Contact information e.g.
Mobile phone number, email address and postal address) pamoja na uchaguzi wa
masomo (Programme selected).
Waweza kuingia katika linki hii hapo chini na kuona majina
ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika maombi yao kwa TCU
http://www.tcu.go.tz/uploads/
file/LIST%20OF%20APPLICANTS%
20FOR%202012-2013% 20ADMISSIONS%20WITH%20MISSING% 20INFORMATION.pdf
Pia waweza kutembelea linki zifuatazo na kushuhudia majina
ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika maombi yao kwa bodi ya mikopo;- http://www.heslb.go.tz/index.
php?option=com_content&view=
article&id=365&Itemid=66
http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=366&Itemid=67
http://www.heslb.go.tz/index. php?option=com_content&view= article&id=367&Itemid=68
post graduate;- http://www.heslb.go.tz/index.
php?option=com_content&view=
article&id=363&Itemid=65
Hata hivyo taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa
sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo
waliyotoa. Kwa taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz
na www.tcu.go.tz
0 comments:
Post a Comment