Alakiwa kama mfalme
Gari lake lasukumwa na wanaharakati
Kiongozi wa
jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa amebeba maua,
na kuzungukwa na Madaktari wenzake na wananchi wa kawaida waliofika kumlaki,
mara alipowasili mapema leo Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu
nchini Afrika Kusini. Dk Ulimboka alisema kuwa yuko fiti na anaweza kufanya
shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment