PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Hawa Ngulume afariki dunia


Na Salesi Malula

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Kinondoni na Mbalali, amefariki dunia leo, katika Hospitari ya Lugalo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jodarn Rugimbana katika mahojiano ya simu na mtandao wa wamoja amethibitisha kutokea taarifa za tukio la msiba huo mzito.
Yaaa ni kweli Mheshimiwa Hawa Ngurume amefariki Dunia katika Hospitari ya Lugalo, na taratibu za mazishi zinaandaliwa lakini nikueleze tu kuwa hawa Ngulume sasa ni marehemu.
Anasema Hawa Ngulume, atakumbukwa katika mambo mengi sana, lakini kubwa zaidi ni ujasiri wake kwani watu wa mbarali hawatamsahau hasa aliposimamia zoezi la kuwaondoa wafugaji katika bonde la Ihefu.
Hawa Ngulume, amewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbalimbali hapa nchini, na amewahi kuwa mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya wote hapa nchini, ambapo amefariki akiwa ni mtumishi wa umma aliyestaafu.
Taratibu za kusafirisha mwili wa Marehemu Hawa Ngulume kwenda nyumbani kwao Singida kwa maziko zinaandaliwa.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: