Na Salesi Malula
Watu 11 waishio
maeneo ya Kigogo, Mbuyuni Jijini Dar es salaam, wamefariki Dunia baada ya
kunywa pombe haramu aina ya Gogo, ambapo muuzaji wa gongo hiyo aliyelazwa katika Hospitali ya Amana iliyoko
Ilala amepoteza maisha.
Mwandishi wa Mtandao wa Wamoja akiongea na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mbuyuni katika eneo la Tukio Bw.Mohamed Mnunga alisema, tukio la kufa kwa watu
waliokunywa Pombe kwa mama aliyejulikana kwa jina la mama Ikima Bakari, lilijulikana baada ya mtu
mmoja kufariki Dunia kutokana na kunywa Pombe hiyo ambapo kabla ya msiba
kusafirishwa ndipo matukio ya watu kuzidiwa yalipoanza kujitokeza ambapo watu
walikimbizwa katika Hospitari ya Amana kwa matibabu.
“Tukio hilo limesababisha watu 11 kufariki Dunia na hadi
hivi sasa hata muuzaji wa Gongo hiyo aliyelazwa katika Hospitali ya Amana
kwaajili ya matibabu amefariki,” alisema Mwenyekiti huyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Charles Kenyela alipoulizwa na Mtandao wa
Jamii ya J&M; WAMOJA, juu ya tukio
hilo alisema alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi
zaidi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Wakati huo huo hofu imetanda kwa wakazi wa ameneo hayo ya Kigogo
hasa wale wanywaji wa Pombe haramu ya
Gongo ambao walikunywa kwenye klabu ya mama huyo, kuwa inawezekana watu wengi
wakapoteza maisha kutokana na pombe hiyo kwani watu wengi waliinywa na kuwa yamkini maafa zaidi yakatokea.
0 comments:
Post a Comment