Tangu kitokee kifo cha aliyekuwa
mpambanaji wa Afrika, Nelson Mandela mengi yamezungumzwa na bado yanmaendelea
kuzungumzwa,, Nilikaa kimya nikitafakari
niseme nini juu ya mtu huyu, ambaye kila mmoja anamsemaa vizuri kutokana na
maisha aliyoishiza hapa ulimwenguni,
kidogo nilishindwa kupata cha kuzungumzia, kutokana na na mengi niliyosikia kupitia
vyombo vya habari na mitandao ikiripoti.
Wakati nikiendelea kutafakari niseme nga neno moja juu ya huyu mtu mashuhuri
nikakumbuka neno moja katika Biblia inasema: Kama alivyowekewa mtu kufa mara
moja na baada ya kifo hukumu. (Ebrania 9:27). nikapata lakusema. Mzee madiba naajua huko aliko
wala hata nikisema mazuri kiasi gani hawezi kunisikia, lakini niungana na wengi
kusema, kazi yako umemaliza hapa duniani
hivyo sasa hatuna sehemu na wewe, tangul;ia mbele ya kiti cha enzi.
Ni kweli tunaweza kusema mengi
mazuri juu yako, kulingana tulivyoshuhudia maisha yako ukiwa nasi hapa duniani,
lakini sasa uko peke yako huko uliko ukikabiliana na hakimu mkuu anayepima kwa
haki, akiangalia mwenenndo mzima wa safari yake, kama ni mema au mabaya anajua
yeye.
Ni wakati sasa kwetu tuliosalia
kujitazama kupitia msiba huu mzito, hasa tukijihubiri maisha yetu badala ya
kuendelea kuhuzunika tu bila faida yoyote. Mandela ameacha umati mkubwa nyuma
yake, familia kubwa ambayo sasa macho yote yanatazama nani atafanya nini na
nani atavaa viatu vyake
0 comments:
Post a Comment