PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Wanafunzi 898,881 wa Darsa la saba kufanya Mtiahani Leo


WANAFUNZI 898,881 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza shule ya msingi unaotarajiwa kuanza leo Septamba 19 -20 nchi Nzima. 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema jana kuwa kati ya hao wanafunzi 426,285 (asilimia 47.64) ni wavulana na wanafunzi 468,596 (asilimia 52.36) ni wasichana .

Alisema kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 874,379 watafanya mtihani huo kwa Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya mtihani kwa Kiingereza, lugha waliyoitumia wakati wa kujifunza.

Naibu Waziri alisema wanafunzi 92 wasioona pia wanatarajiwa kufanya mtihani huo na kati ya hao 53 ni wavulana na wanafunzi 39 ni wasichana.

Alisema watahiniwa wenye uono hafifu ambao wanahitaji maandishi makubwa ni 495 kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.

“Mtihani huu kwa mara ya kwanza utafanyika kwa kutumia teknolojia mpya ya Optical Mark Reader (OMR) ambako watahiniwa watatumia fomu maalum za kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kompyuta.

Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya jamii,” alisema Mulugo.

Alisema maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa fomu maalum za kujibia mitihani na nyaraka zote zinazohusu mtihani. 

Aliwaomba maofisa elimu wa mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na mazingira yanakuwa salama na utulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: