PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Mauaji kama haya nchini yahusishwe na Ugaidi!


·         Wote waliouliwa ni wadau wa habari 
·          Muuza magazeti na Mwandishi, kulikoni?
      Na Joseph Herman
      KATIKA mataifa mengi ulimwenguni, na hasa yale yanayoonekana kutetea haki za binadamu, yamekuwa yakipinga vikali vitendo vya kutisha, kutumia nguvu, mauaji na mashambulizi yanayofanywa kwaajili ya kufikia lengo fulani ya kisiasa(Ugaidi).Taifa la Marekani limekuwa mstiri wa mbele katika kuhakikisha kwamba vitendo vinavyohusishwa na Ugaidi, vinakomeshwa kote duniani na mpaka hivi sasa kuna kesi kadha wa kadha zinazoendeshwa na Mahakama ya Kimataifa (ICC) zinazolenga kuajibisha ama nchi au kiongozi aliyetuhumiwakuhusika na mauaji kama hayo.
      Nchi kama ya Rwanda, kuna kesi ambazozinaendelea kurindima nchini humo ambazo baadhi yake zinahusishwa na matukio ya mauaji ya mimbari yaliyotokea miaka ya1994, (Rwanda Genocides), ambapo watu zaidi ya 800, 000, wakiwemo watoto waliuliwa kikatili. Matukio yoyote ya mauji ya kutisha kama hayo,yanaweza kuchukuliwa ama kuhusishwa moja kwa moja na ugaidi kama tafsiri ya neno lenyewe.
      Kwanza kabisa kabla sijaendelea mbele kueleza machache yaliyobeba mengi na machungu yaliyojaa ndani ya moyo wangu, nitoe kwa kifupi maana halisi ya neno Ugaidi, ili nitakapofika katika lengo langu   hasa  kwa yule atakayeguswa nayo asinichukulie kuwa namhukumu mimi bali ajihukumu kwa haki kama ndiye mhusika halali wa jambo hili.
      Ugaidi nini basi?
      Daudi Mwangosi akiadhibiwa na Jeshi la Polisi
      Tafsiri ya Oxford,Kamusi ya   Kiswahili Sanifu. Maneno mapya, maelezo bora zaidi, minyambuo na mifano tele. Toleo la Pili, iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili , Dar es Salaam, wanafasiri Neno hili Ugaidi kama kuwa ni “Vitendo vya kutisha; kutumia nguvu; mauaji na mashambulizi yanayofanywa kwa ajili ya kufikia malengo fulani ya kisiasa.”
      Kwa utafiti wa wanafalsafa wengine duniani wanasema kuwa neno ugaidi kwa lugha ya Kiingereza linafahamika kama Terrorism, ambalo asili yake linatokana na neno la Kilatini terrere, ambalo maana yake ni kuogofya au ogopesha.
      Neno hili limekuwa likitumiwa katika maeneo na matukio mbalmbali  kulingana na hali halisi ya tukio lenyewe, na mara nyingi limekuwa likitumika katika matukio yale yaliyohussishwa na vurugu za kisiasa zilizosababisha mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia kwa kusudi la kutimiza lengo fulani la kisiasa kama fasiri namba moja inavyoeleza kwenye kamusi, na hasa wakati wa mapigano ya kuleta mabadiliko ya maendeleo mapigano au mashambulizi yoyote yaliyosababisha mauaji yalitafsirika kama UGAIDI.

      Kwa mantiki hiyo basi tukio lolote la mauaji linalotokea kwa ghafla katikati ya jamii fulani linaweza kuchukuliwa kama moja ya ugaidi, na hii ndiyo maana leo ninaweza kuwa na ujasiri kutoboa wazi kuwa, mauaji kama haya yanayodaiwa kuhusisha Jeshi la Polisi la Tanzania kwa mujibu wa tafsiri la neno lenyewe yachukuliwe kama Ugaidi nchini, na hakuna sababu ya vyombo vinavyopambana dhidi ya Ugaidi kulifumbia  macho ama kulionea haya. Nadhani hapa wahusika hawawezi kulikwepa hili, kwani matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni nchini tukianza na  vurugu za kisiasa mjini Morogoro ambapo  Jeshi la Polisi wakati likijaribu kuzima maandamano yaliyokuwa yakifanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), raia mmoja asiyekuwa na hatia muuza magazeti Bw. Ally Nzona, alilipuliwa kichwani  na kile kinachosadikiwa kuwa ni bomu na kupelekea kufariki dunia.
      Kutokana na matukio hayo wengi wamelituhumu Jeshi la Polisi kuhusika moja kwamoja na mauaji hayo, kwanza yale yaliyojitokeza Morogoro na Iringa, japo bila kuchelewa jeshi hilo lilionekana kujitokeza haraka kupitia vyombo mbalimbali vya habari  likikanana  kuhusika kabisa na mauaji hayo, huku wengine wakikirushia lawama Chama cha CHADEMA, kwa madai kuwa ni njama  zao tu, kuua mtu ili waichafue Serikali na Jeshi lake.
      Madai yote yaweza kuwa kweli, lakini! haiingii akilini hata kidogo, kuona Jeshi lenye vifaa vyote vya kiuchunguzi washindwe kubaini vyanzo vya vifo hivyo mpaka ete waunde tume. Kana kwambna wao kweli hawakuhusika na tukio lenyewe. Nadhani  ni wakati sasa wa serikali kuliangalia swala hili kwa kina sana, kwani limegusa wanahabari kwa karibu na haliwezi kuvumilika ama kusahaulika kwa haraka katika kumbukumbu za mioyo yao.
      Kwenye matukio haya ya mauaji  mawili, Morogoro na tena Iringa, kwa mwandishi wa habari aliyepoteza maisha kishujaa Bw. Daudi Mwangosi,  kuna migongano ya hoja nyingi kati ya  Jeshi la Polisi, Waandamanaji, CHADEMA,  wananchi, mtu asiyefahamika(Gaidi), ama marehemu mwenyewe japo yeye amesitiri siri ambayo hata hivyo Mungu ndiye anayeweza kulifumbua, kwangu mimi na wewe ni fumbo. Migongano hiyo ni; nani mhusika mkuu na matukio yenyewe? Nani anayepaswa  kuwekwa lupango alisaidia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wake? Hiki ndicho kitendwawili kikubwa, ambalo mimi na wewe tunalingojea lifumbuliwe.  Kwa taarifa na tuhuma za awali zilisukumwa moja kwa moja kwa Jeshi la Polisi, hivyo wangefanya jambo la busara kujisogeza wenyewe nondoni, ili wajisidie wenyewe kufanhya uchunguzi huku wakitafuta watuhumiwa wengine.
      Serikali ikumbuke kwamba, mauaji haya yanayofanana sana na ya kigaidi, kama hayatachukuliwa hatua stahiki mapema wajiandae kupokea hukumu ambayo Mungu ndiye anayeiandaa kwa awamu nyingine ijayo ikisimama juu ya damu za mashujaa hao waliotutangulia mbele ya kiti cha haki.
      Kila mtu aliyeumbwa na Mungu ni shahidi wa nafsi yake mwenyewe, bomu kama bomu halina nafsi linabebwa na mtu aliye na nafsi hivyo aliyesababisha tukio hilo yupo na anafahamu kile alichokifanya na kwa makusudi gani, na kwa maslahi yapi. Ni wakati  sasa kwa wachunguzi wa swala hili kutumia vifaa vya kisasa vya kiuchunguzi (Crime Scene Products), ili kubaini watuhumiwa wa mauaji hayo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Wachunguzi wa jambo hili waige mfano wa Polisi wa Afrika ya Kusini ambao walifanikiwa kuwatia mbaroni zaidi ya watu 150, wakati wa uchunguzi wa mauaji ya wachimbaji wadogo 34 wa migodi. 
      Na kwamba yoyote atakayebainika kuhusika na matukio hayo, awe ni mtu binafsi, Jeshi la Polisi ama Chama chochote cha Kisiasa, ashughulikiwe kikamilifu  kama gaidi na asifumbiwe macho kwa vile anahatarisha amani ya nchi hii. Nathamini Jeshi la polisi litakuwa makini kushughulikia swala hili hasa wakati huu wa majonzi mazito kwa wanahabari wa nchi hii pamoja na familia ya wafiwa wote wa pande zote mbili. Wakati wanaposhughulikia swala hili serikali ni lazima itambue kuwa, unapomchimbia kaburi mwenzio leo ujue na wewe wapo wanaojiandaa kukuchimbia lako kesho. Marehemu wote wawili walikuwa kama tulivyo leo, walipanga waliishi na familia kama tulivyo sasa, lakini tutambue kuwa kesho tutakuwa kama walivyo leo kwa namna yoyote ile. Mabadiliko ni dhahiri kwa kila jambo chini ya jua, liwe linahusu taifa ama mtu binafi. Tuwe makini na hili!
      Share on Google Plus

      About Unknown

      0 comments: