· TANESCO huduma kwa wateja yawatafuna
Salesi Malula na Joseph Ongong’a
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamekua katika misururu mirefu kununua Umeme wa Luku kufuatia tangazo lililotolewa na shirika la umeme Tanesko kuwa linataka kubadilisha mfumo wa luku.
Mamia ya wakazi wa jiji la dare s salaam walionekana kupanga foleni kubwa wakiwa na lengo la kupata umeme.
Kituo cha Big Bon kilichoko maeneo ya Zakhem mbagala jijini Dar es Salaam, ndio kilionekana kuwa na watu wengi zaidi ambao walikuwa wakihitaji umeme.
Zoezi la mfumo wa mabadiliko ya LUKU kwa mujibu wa TANESCO litachukuwa muda wa siku tatu, ambapo kwa siku ya leo wakazi wa jiji la Dar es salaam, walihaha katika vituo hivyo kutafuta umeme wa huo ili kujihami na mfumo wa mabadiliko ambao unatarajiwa kuanza kesho.
Hata hivyo wengine wameilalamikia huduma mpya iliyoanzishwa na Shirika la TANESCO, kwa wateja ambayo imekuwa ikiwala pesa hata ipopokelewa. Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa J &M; Wamoja umebaini kuwa, huduma hiyo imekuwa ikikata pesa tena kwa kasi sana hata kama hautafanikiwa kuzungumza na Mhudumu wa TANESCO.
“Ndugu Mwandishi, nilipiga simu namba 0222194400, lakini niliambulia tu wimbo wa kunishawishi niendelee kusubiri, kuwa nitahudumiwa hivi punde kwakuwa wahusika bado wanawahudumia wateja wengine, lakini nikiendelea kuburudika na mziki uliokuwemo nilisikia simu yangu ikilalamika ikiashiria kuishiwa vocha, nilishtuka lakini nilipoangalia salio nilikuta zote zimelambwa Shilingi 4500, zote,” alisema mteja huyo.
0 comments:
Post a Comment