Wabunge wanatakiwa kuelewa kwamba magomvi, mabishano na vitisho kati yao yanaweza kuhatarisha mstakabali wa amani ya nchi hii kama hawata kuwa makini katika hilo. Kwa muda nimekuwa nikifuatilia vikao vya Wabunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo nimekuwa nikishuhudia mabishano yasiyo kuwa ya msingi, hata wakati mwengine unawakuta wabunge wakirushiana maneno makali, yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi hii. Ningewaomba Wabunge ambao ndiyo wawakilishi wetu serikalini kuwa makini kwenye hilo ili waweze kuilinda na kuitunza amani ya nchi yetu.
CHONDE CHONDE WABUNGE MUWE MAKINI MPENDANE KAMA NDUGU MOJA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment