CASFETA TAYOMI WAITEKA CHALINZE
·
Wasaka
watu nyumba kwa nyumba
·
Zaidi
ya watu 400 wakimbilia kwa Yesu
·
Askofu
Wa Jimbo awaunga mkono
Na Joseph H. Ongong’a
Jumuiaya wa Wanafunzi waliookoka
wa Chuo Kikuukcha Dar es Salaam wa CASFETA TAYOMI, wamefanya mapinduzi
makubwa huko Chalinze Mkoa wa Pwani, kwa
kuwavuta watu zaidi ya 400 kwa Yesu wakati wa mkutano wao wa Injili uliofanyika wiki iliyopita katika
viwanja vya NMC Bwirungu, ambapo katika mkutano huo, wengi wamepokea uponyaji
na kufunguliwa kutoka katika vifungo malimbali vya
shetani.
Akiongea na gazeti hili katika
eneo la viwanja hivyo, Mchungaji Msaidizi
wa Kanisa la TAG Mabibo Spiritual Centre, Nimrod Swai, alisema kuwa,
katika mkutano huo uliodumu hapo kwa wiki moja ulikuwa na matunda makubwa sana,
kwani vijana hao walifanya kazi kubwa ya kuhubiri injili Usiku na mchana huku
wakiwasaka watu nyumba kwa nyumba na
kufanikiwa kuwapata wengi.
Alisema kuwa kwa ushirikano
mkubwa Vijana hao, waliweza kufanya kazi usiku na mchana, ambapo kwa wakati wa asubuhi
hadi mcha walifanya kazi ya kuzunguka mitaani kushuhudia, jioni walihubiri
katika viwanja vya mkutano na usiku
walifanya uinjilisti kwa njia ya kuonesha sinema.
Alisema pamoja na mkutano huo
lakini pia Vijana hao waliokuwa na muda wa kuonesha utalaamu wao katika ubunifu
wa mambo mbalimbali kwa kutumia ngamizo, kama njia mojawapo wa kujitafutia pesa
kwa ajili ya kupanua huduma yao ya uinjilisti.
Hata hivyo pamoja na mkutano huo
Mchungaji Swai alisema kuwa, kulijitokeza changamoto mbalimbali na vikwazo
wakati wa mkutano huo kanma vile watu wasiojulikana kujaribu kuchoma moto
mazingira ya shule ya Chalinze Sekoindari walipopiga kambi kwa lengo la kudhoofisha mkutano huo na
kuwafukuza washuhudiaji.
“Tunashukuru Mun
Askofu wa Jimbo la Mashariki
Kaskazini, Kanisa la TAG, GDO Massawe, katikati, akiwaunga wanafunzi hao mkono
kwa kuwasaidia kazi ya mapishi
gu kuwa, pamoja na vikwazo vyote hivyo lakini
aliweza kutushindia na mkutano wetu kuendelea kama kawaida,” alisema Swai.
Kwa upande wake Askofu wa TAG
Jimbo la Mashariki Kaskazini, Geofrey Masawe, alipongeza kazi kubwa inayofanywa
na vijana hao wa Chuo Kikuu sehemu ya mlimani , wa kuhubiri injili ambapo alitoa wito kwa Wanafunzi wote wa Elimu
ya juuu wa vyuo vingine kuiga mfano huo
Kwaya ya wanafunzi waliookoka wa
vyuo vikuu(CASFETA TAYOMI) wakimsifu Mungu huko Chalinze(Picha na Joseph
Herman)
“Vijana wakimtumikia Yesu kama
hivi inatia moyo sana, hii ni changamoto kubwa kwetu, Mungu atatudai zaidi kama hatutafanya
kazi yake kwa bidii kama wafanyavyo Vijana hawa,” alisema Askofu Masawe.
Akihubiri wakati wa mkutano huo,
Mwenyekiti wa Vijana hao Mwinjilisti Pascal Christian, ailiwataka watu wa eneo
la Bwirungu Chalinze kugeuka kutoka kwenye njia zao mbaya na kumrudia Mungu,
wakikumbuka kuwa siku moja wataicha dunia na kusimama mbele ya kiti cha hukumu
ya Mungu.
0 comments:
Post a Comment