Tuko kwenye dunia ambayo kila
kukicha kuna tafiti mpya au tunakumbushwa yale ambayo tunatakiwa
kuyazingatia kila siku kwenye maisha na ninafahamu Watanzania wengi huchelewa kufika nyumbani na hata kula chakula cha jioni.
Kwenye mida ya saa mbili usiku hivi
ndio utatukuta mezani lakini Wataalamu wanasema tunakosea kula chakula
time hiyo maana chakula kizito mwisho kula ni saa kumi na moja jioni na
baada ya hapo ni vile vilainilaini tu.
Unaambiwa kuanzia saa kumi na moja
jioni na kuendelea hautakiwi kula chakula kizito bali vile vyepesi tu
mfano Juice maji na matunda sababu ukila chakula kizito na kulala muda
mfupi baadae kitazuia ufanisi wa msukumo wa damu mwilini na mwisho wa
siku ndio tunapata magonjwa ya shinikizo la damu.
0 comments:
Post a Comment