PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

Dk. Mtokambali katika hili umesimamia kweli!

Na Joseph O. Herman

WAKATI ahadi ya  Kiongozi wa Kanisa la Last Glory, Askofu Baxilcus Ezekiel Mapumba, ikingoja kutimizwa kama alivyotaka, kupitia utabiri wake, juu ya mmoja wa watangaza nia wa Chama cha CCM, utabiria ambao hata hivyo   sasa dalili zake zinaelekea kuzama,  Matamko, mahubiri na maonyo ya Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God, Dk. Barnabas Mtokambali linabaki kuwa somo kuu kwa viongozi wa kiroho na dini hapa nchini. 
Askofu Mkuu wa TAG Dk. Barnabas Mtokaambali
Endapo kama Askofu Ezekiel Mapumba, na wenzake ambao tabiri zao hazitimii kama wanavyotegemea walipaswa kutekeleza yale aliyokuwa yakinenwa na kiongozi mwenzie wa Kiroho Wa kanisa la TAG, kupitia vyombo mbalimbali vya habari, na maeneo mengine, kamwe wasingeangukia katika fedheha kubwa kama hii.
 Manabii ni wajanja sana wa kuhepa mishale kama hii, pale wanapojigundua kuwa, matarajio ya tabiri zao hazikwenda sawaswa, lakini sijui katika hili itakuwaje kwa  Askofu Mapumba, na wenzake wanaofanana naye,   hebu soma  utabiri huu, nainukuu kama ilivyoripotiwa na gazeti moja na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ikisomeka: “Lowasa asipokuwa Rais 2015 mniue,” Askofu.
Kwa yale yaliyojiri Dodoma kuanzia Julai  nane hadi 12, 2015, amabapo mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi, kilimchagua Dk. John Pombe Magufuli, kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais, na kuwaacha watabiriwa imezidi kuwaaweka panbaya watabiri.
Ningetamani kuwasikia baada ya uchaguzi huo wa hatua za awali kupita,  wanaelekeza tena wapi utabiri wao, lakini kama nijuavyo wengine sasa wameanza kumtafuta Mheshimiwa Magufuli ili waanze tena kutupa karata zao za utabiri kwake.
Utaanza kusikia bila aibu, Magufuli ni Chaguo la Mungu, ohoo! mara Mungu amesema hakuna atakaye simama naye, hizi ni kauli ambazo zitaanza kujitokeza mapema sana. Mara nyingi Dk. Mtokambali amekuwa akihonya hilo, na zaidi amekuwa akisisitiza waumini na wachungaji kujitokeza kwenda kupiga kura ili kutenda haki na siyo kuwa sehemu ya malumbano ya kisiasa.

Harakati  hizi za kuwania urais kupitia vyama mbalimbali vya kisiasa hapa nchini, baada ya kutangazwa  kwa wale watakaowakilisha vyama hivyo  kuwania nafasi za ugombea urais,  umewaweka baadhi ya viongozi wa dini njia panda, kutokana na  kile kinachoonekana kwamba matarajio ya utabiri walizotoa kwa baadhi ya wagombea katika ngazi za vyama, kushindwa kutimia.
Kama ilivyo kawaida , kwa baadhi watumishi wa Mungu  kujitokeza kutoa unabii kwa wagombea,  wakati wa hekaheka za kampeni za uchaguzi,  wakiwatabiria ushindi na wengine kuweka ratiba za maombi kwa ajili ya wagombea, jambo ambalo limekuwa likiwafedhehesha mara tu baada ya utabiri wao kushindwa kutimia, tofauti na matarajio yao.
Nukuu na matamko ya Dk. Mtokambali, wakati wa mbio za uchaguzi na baadhi ya matukio ya kitaifa na mengine ya kijamii   wakati wa  mahubiri yake, yanazidi kuleta chachu kwa baadhi ya viongozi wengine wa kiroho, na kidini, kwani  amekuwa akitumia madhabahu, kumhubiri Mungu aliyehai, kufundisha, kukemea na kuwaonya watumishi kuacha kujiunga na kundi lolote la kisiasa na  kutimiza kusudi la wito wao, jambo ambalo ni la msingi sana kwa mstakabali wa kutunza amani ya nchi hii.
Alipokuwa mgeni rasmi kwenye moja ya uzinduzi wa albamu ya mwimbaji nuli wa mziki wa injili, Jenifa mgendi, Dk. Mtokambali katika hotuba yake aliwakemea waimbaji wa nyimbo za Injili wanaotumia karama zao kupigia debe viongozi wa siasa, jamboambalo alionekana kukerwa nalo sana.
Dk. Mtokambali alitoa hotuba ndefu ambayo alitaka lichapishwe kwenye vyombo mablimbali vya habari, ili kuonesha msimamo wake huo. Hotuba hiyo ilichapishwa katika gazeti la Jibu la Maisha.
Kiongozi mmoja  msomi wa kiroho Dk. Rejoice Ndalima, nilipomhoji kuhusu jambo hili naye aliunga mkono misimamo ya Dk. Mtokambali na TAG, ambapo alisema: Hebu jiulize itakuwaje, kwa wale ambao walitabiriwa kuwa Mungu amesema, kuwa ni lazima wtapita, halafu wasipite, je, wataendelea kuwa na imani na kanisa baada ya matarajio yao kushindikana? Na je kwa maumivu makali waliyonayo  kwa sasa watakuwa tayari tena kurudi na kumshukuru Mungu, kwa matokeo waliyopata.
Yeye alisema anashari ili kulinda heshima ya kanisa watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwa waangalifu na kauli zao, wawe wastahimilivu na wasiwe na misisimko,  wala wasikubali kuyumbishwa na upepo wa kisiasa. Yeye alishangazwa na wale waliojitokeza mapema kwenye makundi ya kisisa, jambo ambalo alisema kuwa limezidi kuwapotezea sifa ya utumishi wote walioonekana kwenye vyombo vya habari wakiunga kundi Fulani.
Aliupongeza msimaamo wa TAG  ambapo alisema Tofauti na kama ilivyo kwa baadhi ya watumishi wengine wa Mungu, Kiongozi Mkuu wa kanisa hilo Dk Mtokambali, yeye amekuwa akitoa matamko mbalimbali, yanayolenga kuwaonya watumishi wa Mungu hasa wa kanisa hilo la TAG, kutojiunga kabisa na makundi ya  kisiasa, kwa kile anachosema kuwa, ndio msimamo mzuri wa kiongozi wa kiroho.
Dk.Mtokambali katika hutuba na kauli zake ambazo mara nyinggi zimekuwa zikitoa matokeo chanya, ikiwa ni pamoja na  ile aliyotoa mwaka 2011, dhidi ya  Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo na uponyaji wake wa kikombe cha babu, ali kuwa wa kwanza kupinga na kuonya watumishi na waumini wa kanisa hilo kuhusina na uponyaji huo feki.
Ukweli usiofichika ni kwamba, kikombe cha babu wa Loliondo kimeacha kilio kikubwa kwa wale waliokitumia, pamoja na kwamba uponyaji huo ulishabikiwa sana na viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi wa dini waliouhusisha na nguvu za Mungu, lakini takwimu zinaonesha kwamba wagonjwa weni waliokitumia walipoteza maisha. Hakuna anayekionggelea hicho kikombe hivi sasa.
Mgonjwa mmoja aliyethubutu kuacha dawa za ARV, na kudhani ataponywa na kikombe cha babu anasimulia kwenye mtandao wake wa jamii unaojulinakana kama mwanasosholojia.blogspot.com, anasema kuwa nusura afe baada ya kutumia kikombe cha babu. Anasema kuwa alilazimika kurudia dawa zake za ARV ili uzima wake umrudi lakini marafiki zake watatu walipoteza maisha yao.
Misimamo ya kanisa las TAG kwa mambo kama haya, yameijenggea heshima kubwa, kwani, mchungaji mwema ni yule anayelilinda kundi lisipate madhara, ama mashambulizi ya adui. Hivi ndivyo wafanyavyo viongozi wa Kanisa la TAG, amabao wanakuwa makini na mambo yanayoibuka, hawakurupuki, badala yake husubiri na kuacha Mungu ajitwalie utukufu. Kwa hili ni “big up” na fahari sana kwa kanisa.
Mwana falsafa mmoja Hank Campbell anasema: vita kubwa ya kiroho ni kuwa tamaduni za siasa inaiathiri sana kanisa tofauti na nyakati zilizopita ambapo kanisa liliathiri zaidi siasa. Mwana falsafa huyo anasema kama kanisa litajiingiza sana katika mambo ya kisiasa basi litakuwa limeacha wajibu wake na mahekalu kugeuzwa majumba ya kufanyia kampeni na siyo kuhubiri neno la Mungu lililo hai, jambo alilidai kuwa ni kifo cha kanisa.
  “Kiongozi yoyote wa kanisa hili la TAG kama atabainika  kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa serikali, ama utaonekana kwenye kundi lolote la chama cha kisiasa,  basi acha uchungaji,” amekuwa akisema Dk. Mtokambali na kuongeza: na kama utajiunga na siasa na kuacha kanisa, ukirudi tutakufikiria,  kwa kukujadili na kama atatimiza vigezo tutakupeleka maneo menine kuanza kanisa jipya.”
Siyo hivyo tu bali Mtumishi huyo amewajengea msimamo imara  watumishi wa kanisa hilo, kuanzia wachungaji wa makanisa ya mahali pamoja , waangalizi na kwa maaskofu wa majimbo, jambo ambalo limeiwekea heshima kubwa kanisa la TAG, siyo tu kwa jamii lakini pia kwa Taifa la Tanzania.
Nasema hivi kwa sababu, tofauti na baadhi ya wachungaji wa madhehebu mengine, hasa mitume na manabii ambao  wamekuwa wakionekana katika lunginga na wengine kuripotiwa kwenye vyombo mbalimbali  vya habari, mitandao ya kijamii,  wakiunga mkono makundi ya waombea wa vyama vya kisiasa,  kwa  TAG,  wao wamekuwa wakisisitiza maombi kwa ajili ya amani ya  taifa hili na uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Kanisa siyo jukwaa la  siasa, ni hai kwa ajili ya Mungu, ndivyo mara kwa mara asemavyo kionozi huyo wa kiroho. Lakini jambo linalosikitisha ni kwamba wapo wengine ambao naweza sema kuwa sikio la kufa halisikii dawa, wamekuwa wakitumia madhabahu yao kuwatabiria viongozi wa kisisa na kuwapa tumaini kuwa wa Mungu amesema wanashinda.
Jambo linalotia wasiwasi hapa ni kwamba watumishi hao wa Mungu wamekuwa wakitoa utabiri  kwa viongozi wengi tofauti, jambo ambalo linaibua maswali mengi  kuwa je! Mungu anaweza kutumia watumishi tofauti kutoa tabiri nyini tofauti na tena ambazo hazitimii? Na kama je! Tabiri zote ambazo hazitimii tuziweke kwenye kundi gani?
Kwa msimamo hii ya Kanisa laa TAG kupitia kiongozi wao Mkuu, sasa imefika wakati kwa viongozi wenye wajibu wa juu katika makanisa kuiga mfano huu wa Dk. Mtokambali, na kanisa la TAG, kwani misimamo na maamuzi  yake yanatija kwa kanisa la  BWANA. Siyo sahihi kwa kiongozi wa kidini ambaye yeye ana dhamana  ya kuchunga waumini ambao wao wanatoka kwenye makundi mbalimbali tofauti ya kisiasa na jaamii, kujiunga na kundi lolote. Inaweza ikawa fedheha na kiliabisha jina la BWANA Mungu ambaye wanamtumikia.
 Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho kikwete, akihutubia katika moja ya mkutano wa kidini hapa nchini, alitoa wito wake kwa viongozi wa dini kuacha kujiunga na makundi yoyote ya kisiasa, akisema kuwa viongoziu wa dini wao wabaki kuwa juu kama baba na washauri, wakati viongozi wa kisiasa wakipambana na mambo yao ya kisiasa.
Kauli hiyo ya Mheshimiwa rais, inazidi kuijengea heshima kanisa la TAG, na na misimamo ya viongozi wake, kwa jinsi ambavyo wao wamekuwa wakiendeleza msimamo thabiti wa  kubaki kuwa baba mwenye watoto wengi walio tofauti amabao wote wanahudumiwa bila ubaguzi wowote.
Nimekuwa nikitafakari sana  kauli na maamuzi haya ya kanisa la TAG, hasa nikiyalinganisha na hali inayotokea hivi sasa. Watumishi wengi wa Mungu wamejikuta wakiambulia aibu baada ya kile kilichotokea Dodoma hivi karibuni wakati wa kutafuta mgombea wa urais atakayepeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao Octoba 25 mwaka huu.
Matarajio ya watumishi wengi walioonekana kwenye majukwaa, wakimuunga mkono wagombea fulani wa nafasi hiyo, yalipotea baada ya kushindwa   kuvuka hatua hiyo, kama walivyowatabiria.
Kauli chagua la Mungu, linawatesa sana baadhi ya watumishi wengi, kwani inawezekana wakati mwingine Mungu huwa anasingiziwa, kwa kumlisha maneno binafsi kinywani mwake wakidai kuwa  kasema.
Nadhani  kwa kupitia haya ambayo tayari yametokea viongozi wa kiroho wamejifunza na kutokana na makosa, ni wajibu wo sasa kurejea kwenye mstari wa kiroho na kuacha wanasiasa waendelee kwenye majukwaa yao ya kisiasa. Wao wakibaki kuhubiri kweli ya Mungu kama wanavyofanya wenzao, hasa wakiiga mfano wa TAG.  



Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: