Katika taarifa fupi ya rufaa dhidi kesi ya Nzabonimana, mwendesha mashitaka anaiomba Mahakama ya Rufaa kuachana na uamuzi uliotolewa na mahakama ya awali kuhusu matukio ya uhalifu yaliyofanywa Aprili 15 na 17, 1994 katika wilaya za Nyabikenke na Rutobwe katika mkoa wa Gitarama, katikati ya Rwanda.
Mei 31, 2012, mahakama ya awali ilimtia hatiani Nzabonimana kwa
mauaji ya kimbari,kula njama za kufanya mauaji hayo,uchochezi na
kuteketeza kizazi katika matukio mengine na kumhukumu kifungo cha maisha
jela, lakini aliachiwa huru kwa uhalifu uliofanyika katika maeneo hayo
mawili yanayotajwa na mwendesha mashitaka.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka katika rufaa yake ya Septemba 12,
2012, anadai kwamba majaji wa mahakama ya awali wamekosea kisheria kwa
kumwona Nzabonimana kuwa alichochea tu mauaji yaliyofanyika katika ofisi
za wilaya ya Nyabikenke Aprili 15, 1994, badala ya kumtia hatiani kwa
kushiriki au kuamuru kufanyika kwa mauaji hayo.
Mwendesha mashitaka anadai kwamba majaji wangemtia hatiani
Nzabonimana pia kwa kosa la kusaidia na kuunga mkono mauaji dhidi ya
Watutsi katika wilaya ya Rutobwe Aprili 17, 1994, kwa kusababisha
kuachiwa huru watuhumiwa wa mauaji waliotiwa kizuizini na maafisa wa
serikali za mitaa kutokana na vitendo vyao. Lakini majaji walimwachia
huru kwa kosa hilo kwa maelezo ya kukosa ushahidi wa kutosha.
Kwa upande wa Kapteni Nizeyimana, mwendesha mashitaka anataka atiwe
hatiani pia kutokana na nafasi yake kama kiongozi wa askari waliodaiwa
kutenda uhalifu kwenye Chuo Kikuu cha Butare na Hospitali ya Butare,
Kusini mwa Rwanda.
Juni 19, 2012, majaji wa mahakama ya awali walimtia hatiani
Nizeyimana kwa mauaji ya kimbari,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa
kivita katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa huo wa Butare na kuhukumiwa
kifungo cha maisha jela.
NI/FK
© Hirondelle News Agency
© Hirondelle News Agency
© Agence Hirondelle
0 comments:
Post a Comment