Kufuatia mgomo wa walimu uliokuwa ukiendelea kote nchini
wa kuishinikiza serikali iwatimizie
walimu mahitaji yao yote, raisi wa chama
cha walimu tanzania Gration Mkoba, amewataka
walimu nchini kusitisha mgomo huo moramoja na kurejea kazini ili kuepuka mambo mbalimbali yanayoweza kuhatarisha amani yaanchi, ikiwa ni pamoja na kurudisha
nyuma maendeleo ya elimu nchini.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mugabe Manispaa ya Kinondoni jiji Dar es Salaam, wakiwa nje ya madarasa baada ya walimu kugoma kufundisha. (Picha na Samwel Thomas) |
Mkoba amebainisha kuwa, madai
ya walimu yalikuwa ya haki,
lakini hawana budi kusitisha mgomo huo, kutokana na hukumu iliyotolewa jana na
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya kazi,
kuwataka wasitishe mgomo huo, hukuikiwahimiza kuwalipa fidia wanafunzi
baada ya kutokea kwa mgomo huo.
Aidha akizungumzia
suala la kuwalipa wanafunzi fidia ambao
ndio wamekuwa waadhirika wakubwa wa mgomo huo, amesema kuwa wanasubiri kauuli
ya serikali iseme ni kiasi gani kinatakiwa kufidiwa , ikiwa ni pamoja na kuwa na
ufafanuzzi wa kutosha.
Akizungumzia suala la chama hicho kukata Rufaa,Rais huyo amesema kuwa, watakaachini na Mwanasheria wao,
ili kufanya mazungumzo kwa lengo la
kupata uamuzi wa kukata rufaa au kuto kata.
Mgomo wa walimu nchini
ulioanza mapema wiki iliyopita , umefikia tamati leo baada ya raisi wa
chama hicho , kutangaza rasmi kikomo cha mgomo huo, ambao kwa sehemu moja ama
nyingine umepelekea wanafunzi kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Samwel Thomas
0 comments:
Post a Comment