PATA HABARI/MAKALA ZA UHAKIKA

+255-767-402-396

UTEUZI MWINGINE WA RAIS MAGHUFULI LEO AUGUST 24,2016

August 24 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rashid Othman ambaye amestaafu. Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Aidha, Rais Magufuli amemteua Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye. Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments: